Kilo 2,584 dawa za kulevya zateketezwa Dar

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na  Dawa za Kelevya (DCEA), imeteketeza  kilo 2,584.55 za dawa za kulevya.

Kazi hiyo imefanyika leo Desemba 21,2022, ambapo dawa hizi  zinajumuisha kilo 569.25 za heroin, kilo 15.3 za cocaine na tani mbili za bangi na mirungi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Kamishna Jenerali,  Veronica Matikila amesema uteketezaji huo umefanyika kufuatia kumalizika kwa mashauri ya dawa za kulevya katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, na Mahakama za Hakimu Mkazi za Kisutu, Kibaha Pwani pamoja na Mahakama za Wilaya ya Kinondoni, Ilala, Temeke na Kigamboni.

Amesema, dawa za kulevya zilizoteketezwa leo zimehusisha mashauri ya kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2022.

 

Habari Zifananazo

Back to top button