Kiongozi mbio za mwenge ataka kasi ukusanyaji mapato

TANGA: KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ismail Ali ussi amezitaka Halmashauri nchini kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato sambamba na kuzingatia ubunifu wa vyanzo vipya na fedha hizo kutumia kwa ajili ya kufikisha huduma za kijamii kwa wananchi.

Rai hiyo ameitoa wakati Mwenge wa Uhuru ulipoweka Jiwe la Msingi katika vibanda vya biashara 12 vilivyopo katika Halmashauri ya Lushoto ambavyo vinatarajiwa kuingiza mapato ya ndani ya Sh milioni 19.2 kwa halmashauri hiyo.

Mwenge wazindua mradi wa bil 2.7/-

Kiongozi huyo amepongeza ubunifu uliofanywa Lushoto ya kubuni vyanzo ambavyo vitasaidia kuongeza mapato na kuboresha huduma Kwa jamii.

“Dhamira ya serikali yetu ni kuhakikisha mapato ya ndani ya halmashauri yanatumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo itasaidia kusogeza huduma Kwa wananchi hivyo ubunifu huo unastahiki kuigwa na halmashauri nyingine “amesema kiongozi huyo.

Mbunge wa Jimbo la Lushoto Shaban Shekilindi amesema kuwa inatambua umuhimu kuongeza makusanyo ya mapato, ndipo ikabuni mradi wa ujenzi wa vibanda 12 vya biashara.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button