Mwenge wazindua mradi wa bil 2.7/-

Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa maji wenye thamani ya sh bilioni 2.7 ambao utahudumia wakazi zaidi ya 4000 katika Kijiji cha Funta na Manga katika Halimashauri ya Bumbuli mkoani Tanga.

Mradi huo unaosimamiwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) umekuwa mkombozi wa kumaliza changamoto ya ukosefu wa maji ya uhakika kwa wananchi hao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mradi huo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ali Ussi amewataka wananchi hao kuendelea kutunza na kulinda vyanzo vya maji Ili mradi huo uwe endelevu.

Mbunge wa Bumbuli January Makamba amesema kuwa maendeleo hayo ni jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wananchi hususan wa vijijini wanaondokana na shida ya uhaba wa maji safi na salama.

“Sasa wananchi wataweza kufanya shughuli zao za kimaendeleo na kujiongezea kipato kwani ule muda wa kusubiri maji haupo tena kwa sababu yanapatikana kwa wakati , “amesema Makamba.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button