Kisiwa cha Lundo, historia ya ukatili iliyogeuka Fahari ya utalii

Kisiwa cha Lundo ni kisiwa kidogo chenye ukubwa wa hekta 20 kilichoko katikati ya Ziwa Nyasa, takribani mwendo wa dakika 45 kwa boti kutoka mji wa Mbambabay au dakika 10 kutoka Kijiji cha Lipingo, kata ya Lipingo Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma.

Kisiwa hicho mbali ya kuwa kivutio cha utalii wa wanyama na aina nyingi za ndege pia kimebeba historia kubwa inayogusa nyoyo za wengi na kufunza watu kuhusu kipindi kigumu cha historia ya Tanganyika katika eneo hilo.

Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma inaeleza kuwa Lundo si tu kisiwa, bali ni ukumbusho hai wa athari za vita na ukoloni.

Inaelezwa kuwa baada ya Vita ya Majimaji iliyodumu kati ya mwaka 1905 hadi 1907, wakoloni wa Kijerumani walikifanya kisiwa hicho kuwa sehemu ya kuwahifadhi watu waliopata ulemavu kutokana na ugonjwa wa ukoma.

Kuanzia mwaka 1908, wagonjwa wa ukoma walikuwa wakipelekwa katika kisiwa hicho, mbali na jamii zao, kwa lengo la kuwatenga na kuzuia maambukizi, lakini pia kwa sababu ya hofu na unyanyapaa uliokuwa umejengeka dhidi ya ugonjwa huo.

Miaka mingi baadaye historia hiyo isiyopendeza inafunikwa na uamuzi wa kukifanya kisiwa hicho kuwa Hifadhi ya wanyama na kivutio cha watalii.

Mwaka 2021 aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Chritima Mndeme aliwaagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyampori Tanzania (TAWA) ambao ndiyo wasimamizi wa kisiwa hicho katika uhifadhi, wapeleke wanyamapori katika kisiwa hicho ili kiwe hifadhi na kivutio cha utalii.

Mndeme alisema hatua hiyo ilikuwa na lengo la kuongeza vivutio kwa watalii na kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana wilaya ya Nyasa ambayo kwa wakati huo ilitangazwa kuwa kitovu cha utalii cha Mkoa wa Ruvuma.

Kufuatia agizo hilo kwa kushirikiana na wadau wa utalii mkoani humo, Mshauri wa Maliasili na Utalii Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anasema walitekeleza kwa kuanzisha hifadhi ya Mbambabay ambayo inajumuisha visiwa vya Lundo, Mbambabay na milima ya Mbamba, Tumbi na Ndengere wilayani Nyasa.

Challe anabainisha ukubwa wa eneo la Hifadhi ya Mbambabay kuwa ni hekta 597 zinazojumuisha maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori na ndege na milima.

Anataja maeneo ya uhifadhi katika eneo hilo kuwa ni mlima Mbamba wenye hekta 40, mlima Tumbi wenye hekta 110, kisiwa cha Mbambabay chenye hekta 27 ambacho ni maalumu kwa utalii wa kuona ndege na kisiwa cha Lundo chenye ukubwa wa hekta 20 ambacho Tawa imepeleka wanyamapori.

Mhifadhi katika kisiwa cha Lundo, Maajabu anaelezea kuhusu kisiwa hicho na vivutio vya utalii vinayopatikana ndani yake.

“Hifadhi hii iko chini ya uangalizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), na kisiwa kiko ndani ya ziwa Nyasa katika Bonde la Ufa,” anasema.

“Hifadhi ina wanyamapori rafiki jamii ya swala, sungura pori, kakakuona, kuna ndege wengi ambao wengine ni wa hapa hapa na wengine wengi ni wahamiaji,” anaongeza.

Anasema inapofika mwezi wa tisa hadi wa pili kisiwa cha Lundo kinapokea ndege wengi kutoka maeneo tofauti hususani bara ya Ulaya.

“…tunapokea ndege wengi sana ambao wanakuwa wamezunguka kisiwa, wanahamia kutoka mabara ya Ulaya na maeneo mengine ya nchi.”

“Hifadhi yetu pia ina Samaki wa urembo, kuna aina karibu 400 za Samaki wa urembo wanapatikana katika eneo hili, …pia kuna Samaki aina mbili ambao wanapatikana katika kisiwa hiki cha Lundo peke yake, hawapatikani katika eneo linguine lolote duniani,” anasema.

Anataja aina ya utalii unaoweza kufanyika katika hifadhi hiyo kuwa ni utalii wa kuona wanyamapori, utalii wa kuvua Samaki, utalii wa kuona ndege, utalii wa kuogelea, kutembea ndani ya hifadhi pamoja na utalii wa kuendesha boti.

“…Mtalii akitaka kufanya utalii wa kuendesha boti ziwani tunamwezesha kufanya hivyo.”

Alitaja wanyama wanaopatikana katika hifadhi hiyo ambao ni wanyamapori rafiki jamii ya swala, kakakuona, digidigi sambamba na ndege wa aina mbalimbali wa asili na wahamiaji.

Alisema mbali na kuona wanyama wageni wanaweza kufika na kuweka kambi kwa ajili ya matukio mbalimbali ikiwemo fungate na ziara za vikundi mbalimbali.

“Kwa hiyo tunawakaribisha ndugu jamaa na marafiki waje kufanya utalii katika kisiwa cha Lundo. Lakini ni eneo zuri ambalo linafaa kwa wanandoa kufanya fungate na wanaotarajia kufunga ndoa kupiga picha za kabla ya kufunga ndoa, familia na marafiki,” anasema.

“Hifadhi yetu pia ina maeneo ya uwekezaji kwa hiyo tunakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza kambi za mahema na uwekezaji wa boti za kitalii katika maeneo haya ya ziwa Nyasa na Mbambabay,” anaongeza.

Mbali na vivutio hivyo vya utalii ndani ya kisiwa cha Lundo, jambo lingine lenye kuvutia ni  mandhari nzuri ya mawe yaliyozunguka kisiwa hicho na yale yaliyo chini ya maji.

Iko miamba mingine ambayo imetokeza juu ya maji katikati ya ziwa na kutengeneza mandhari ya kuvutia wakati boti zinapotembea kwenye maji.

Sambamba na hayo unapokaribia ufukweni unakutana na hali tulivu yam aji masafi yanayowezesha mtu kuona vitu vyote vilivyopo ardhini ikiwemo mawe ya ukubwa na maumbo tofauti yenye kuvutia.

Ni usafi huo ndiyo ndiyo unaowezesha samaki wa urembo kuonekana kwa urahisi na katika hali ya kuvutia chini ya maji.

Shuhuda za wageni

Ofisa Mhifadhi wa Hifadhi ya Wanyamapori ya Nyerere Kanda ya Kusini, Emannuel Shango anasema amefurahia safari yake utalii katika kisiwa cha Lundo na amejifunza mambo mengi ambayo hakuyajua awali pamoja na kufurahia mandhari nzuri ya ufukwe wa ziwa Nyasa na kisiwa hicho.

“…tumejifunza vitu vingi, tumeona Samaki aina tofauti, nimefurahi sana,” anasema Shango.

Naye Joshua Laizer anasema “Nimebahatika kufika kisiwa cha Lundo hapa Mbambabay, wilaya ya Nyasa, nimejionea vitu vizuri, mandhari nzuri, kisiwa kizuri ambacho kina wanyamapori kama swala, nimeona ndege wa aina mbalimbali, ndege wanaokula Samaki na aina mbalimbali ya ndege wadogo wanaokula wadudu. Kisiwa ni kizuri,” anasema.

Anatoa wito na hamasa kwa watanzania wote kutembelea kisiwa cha Lundo ili nao wajionee Fahari ya utalii iliyomo ndani yake.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Getting paid Every month more than $25,000 by doing very simple Online job from home.i m doing this job in my part time i have earned and received $25861 last month .I am now a good Online earner and earns enough cash for my needs. Every person can get this Online job.follow details on this website…

    Go Here——➤ http://www.get.money63.com

  2. I get paid over $130 1 to 3 hours working from home with 2 kids at home. I never thought I’d be able to do it but my best friend earns over $27k a month doing this and she convinced me to try. The potential with this is endless.

    Heress———–> http://www.best.work43.com

  3. I honestly thought most online jobs were fake, but this one turned out real. I’ve been doing it for 3 weeks now, just from home, and it’s already paying me $1070+ weekly. If you’re curious, I’ve shared all the info on my site Might be useful for someone serious.
    .
    Open This…. …….. http://Www.Work84.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button