Kitabu uendeshaji data, mipango ya mazingira chazinduliwa

KITUO cha Ubora cha Kanda cha  Bioanuwai, Misitu, na Usimamizi wa Mifumo ya Mazingira ya Bahari katika Mashariki na Kusini mwa Afrika (RCoE-ESA), kinajivunia kuzindua Kitabu cha Ramani cha RCoE-ESA, inayotumika  kusaidia uhifadhi unaoendeshwa na data na mipango endelevu.

Kitabu hicho kina maudhui mengi ikiwemo mada, inayoangazia maeneo yenye bioanuwai, uchambuzi wa kina wa maeneo yaliyolindwa na kuhifadhiwa na mitandao ya uhifadhi wa kimataifa katika nchi 24 za Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Kupitia ramani za ubora wa juu, pia kitabainisha mapungufu  katika ulinzi, na kufanya kuwa muhimu kwa watunga sera, watendaji wa uhifadhi, watafiti na washirika wa maendeleo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu, RCMRD, Dk. Emmanuel Nkurunziza amesema kitabu hicho cha ramani ni chombo kipya chenye nguvu ambacho kinatarajiwa kuongoza vipaumbele vya uhifadhi, uundaji wa sera, na mipango endelevu ya matumizi ya ardhi na bahari.

“Sayansi ya kijiografia ni chombo chenye nguvu cha uhifadhi na maendeleo endelevu. Kupitia upangaji unaoendeshwa na data na ramani ya mfumo ikolojia, tunaweza kurejesha misitu yenye utajiri wa bioanuwai, mandhari ya bahari, ardhioevu na mifumo mingine muhimu ya ikolojia,” amesema.

Amesema kitabu hicho  pia kinaonesha jinsi nchi 24 zinavyopiga hatua kuelekea lengo la mfumo wa kimataifa wa Bioanuwai, unaotaka asilimia 30 ya ardhi na bahari ya dunia kuhifadhiwa kupitia uanzishwaji wa maeneo tengefu (PAs) na maeneo mengine yenye ufanisi za  uhifadhi.

Amesema kwa msaada wa wanachama wa  nchi 20  na washirika wa maendeleo, RCMRD imekua taasisi inayoaminika inayohudumia zaidi ya watu milioni 500 katika Afrika Mashariki na Kusini.

Uzinduzi huo unafanyika wakati wa sherehe za miaka 59 ya RCMRD iliyoadhimisha miongo mitano ya uongozi wa kikanda katika Sayansi ya Geospatial, Uchunguzi wa Dunia, na Ukuzaji wa Uwezo.

“Kwa hakika, imekuwa safari ya miongo mitano kuendeleza ubora wa kijiografia kwa maendeleo endelevu. Kitabu hiki cha ramani ni ushahidi wa urithi huo,” aliongeza Dk. Nkurunziza.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button