Kivurande: Chuki inawaponza wasanii

MSANII wa muziki wa mduara, Hemed Kivurande amesema wasanii wengi hawafikii mafanikio makubwa katika muziki wao kwa sababu ya chuki na kutokupendana baina ya wasanii wenyewe.

Kivurande anasema wasanii wamekuwa wakionyesha chuki za moja kwa moja pindi wanapoombwa msaada wa kisanii na wasanii wenzao.

“Kwenye muziki kuna chuki na kutokupendana kwa wasanii, wengi wao hawapendi wazidiwe hivyo hawatoi sapoti hata ya kushirikishwa ama kusaidia kutoa fursa kwa wasanii wengine ili nao wafikie angalau mafanikio kulingana na sanaa zao,” amesema Kivurande.

Kivurande amesema chuki za wasanii wa ndani ndizo zinazosababisha baadhi ya muziki kushuka ama kuonekana kutokuwa na thamani nchini lakini nje ya nchi unakuwa na uhitaji mkubwa kwa kuwa soko lake ni kubwa mno.

“Mi nawasihi tu tupendane, sanaa ikiwemo muziki inataka upendo na miongozo ya sehemu za kupita hivyo msanii uliyefanikiwa waonyeshe njia wengine nao wafanikiwe wasanii wengi wakifanikiwa hata muziki utakua na utakuwa sehemu ya kuongeza ajira kwa watu wengi,” amesema Kivurande

Habari Zifananazo

Back to top button