Krismasi: Sikukuu ya upendo, matumaini mapya

TANZANIA inaungana na mataifa mengine duniani kufurahia Sikukuu ya Krismasi inayoadhimishwa Desemba 25 kilamwaka, siku inayokumbusha kuzaliwa kwa Yesu Kristo, tukio lenye ujumbe mzito wa upendo, amani na matumaini kwa binadamu wote.

Krismasi ni sikukuu yenye nafasi ya kipekee katika maisha ya waumini wa dini ya Kikristo, lakini pia imeendelea kuwa tukio la kijamii linalokusanya watu wa imani na tamaduni mbalimbali. Ni kipindi ambacho familia hukutana, ndugu na jamaa huimarisha uhusiano, na jamii hujenga mshikamano kwa kusaidiana, hususan kwa wahitaji. Kwa mujibu wa mafundisho ya Kikristo, kuzaliwa kwa Yesu Kristo kunatoa funzo la unyenyekevu na upendo wa dhati.

Yesu Kristo alizaliwa katika mazingira ya kawaida, akionesha kuwa thamani ya mwanadamu haipimwi kwa mali wala hadhi, bali kwa utu na matendo mema. Ujumbe huu unaendelea kuwa muhimu katika jamii ya sasa inayokabiliwa na changamoto za umaskini, migogoro na mmomonyoko wa maadili.

Wakizungumza na HabariLEO jijini Dar-es Salaam baadhi ya waumini wa dhehebu la Katoliki wanasema Sikukuu ya Krismasi inawakumbusha wakristo  wengi kuishi katika matendo mema kwa maisha ya ukristo na kuepuka kufanya dhambi.  “Kuzaliwa kwa Yesu  Kristo  mwanzo wa ukombozi  kwa wakristo,” anasema Benard Shija. “Tunaamini kwa kuzaliwa Yesu Kristo sisi tumepona,” anasema muumini mwingine wa dhehebu la Katoliki  Rose Shirima.

Katika kipindi cha Krismasi, makanisa mbalimbali huendesha ibada maalumu za shukrani, huku waumini wakihimizwa kuishi kwa misingi ya upendo, uvumilivu na kusameheana. Aidha taasisi na watu binafsi hutumia fursa hii kutoa misaada kwa watoto yatima, wazee na makundi mengine yenye uhitaji, jambo linaloendeleza mshikamano wa kijamii. “Sikukuu ya krismasi inatufundisha  pia kukumbuka wengine  wanaohitaji msaada kutoa sadaka ni jambo la kiimani,” anasema Meshack Mkomi. SOMA: Makosa ya kifedha katika Krismasi, Mwaka Mpya

Hata hivyo, viongozi wa dini na jamii wamekuwa wakikumbusha wananchi kuepuka matumizi mabaya ya rasilimali na kusherehekea sikukuu hii kwa kuzingatia maadili, amani na usalama. Wito unatolewa kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanalelewa katika misingi ya heshima na maadili mema, hasa katika kipindi hiki cha sherehe.

“Wakati mwingine watoto  wanatakiwa pia kupewa mafunzo ya dini yetu ya kikristo kufahamu umuhimu wa kutambua  Sikukuu ya Krismas  ambayo  ni muhimu katika maisha  yao,” anasema  Meshack na kuongeza: Aliongezea kuwa, “Lazima wapewe mafunzo ya kufahamu mwokozi wao Yesu Kristo  alizaliwa  kwa ajili yao.”

Wakristo wengi katika Sikukuu ya Krismasi wanatafakari mwenendo wa maisha na kuweka mikakati mipya ya maendeleo binafsi na ya kitaifa. Ni fursa ya kuimarisha umoja, kudumisha amani na kujenga matumaini mapya kwa mustakabali bora wa jamii na Taifa kwa ujumla. Kadri sherehe za Krismasi zinavyoendelea, jamii inahimizwa kudumisha upendo, mshikamano na kujali wengine, si kwa kipindi cha sikukuu pekee, bali kama sehemu ya maisha ya kila siku.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. 6.6 PROGRAMU ZA KIELELEZO

    Mpango Elekezi 2050 umeainisha miradi 14 ya kielelezo. Miradi hii inalenga kuleta mageuzi ya viwanda nchini. Pia, itachochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi wa kijani. Itasaidia kukuza nguvukazi yenye ujuzi na maarifa ya kisasa. Aidha, miradi hii inalenga kuongeza ushindani wa Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa. Miradi hiyo imepangwa kama ifuatavyo:

    NO PROGRAMME

    1 Mageuzi ya Viwanda kwa Ukuaji wa Uchumi

    2 Ujumuishaji wa Sekta ya Madini kwa Maendeleo ya Viwanda na Uchumi wa Kijani

    3 Ubunifu wa Kidijitali na Miundombinu Mahiri kwa Ukuaji wa Siku za Usoni

    4 Ujenzi wa Uhimilivu wa Tabianchi na Uchumi Endelevu wa Kijani

    5 Kuendeleza Miundombinu na Muunganisho wa Usafiri kwa Tanzania kuwa Kitovu cha Kikanda

    6 Mageuzi ya Sekta ya Nishati kwa Umeme Safi na Endelevu

    7 Kukuza nguvukazi yenye Afya, Elimu na Ujuzi

    8 Kuimarisha Utawala Bora, Uwajibikaji na Mifumo ya Udhibiti

    9 Kuendeleza Miji Mahiri na Miundombinu Endelevu ya Mijini

    10 Kuchochea Biashara, Uwekezaji na Upanuzi wa Uchumi

    11 Kupanua Sekta ya Utalii na Uchumi wa Utamaduni

    12 Kubadilisha Sekta ya Kilimo na Uchumi wa Vijijini

    13 Kuboresha Elimu, Utafiti na Ubunifu wa Kiteknolojia

    14 Mageuzi ya Kifedha ya Kidijitali na Jumuishi .

  2. 6.6 PROGRAMU ZA KIELELEZO

  3. 6.6 PROGRAMU ZA KIELELEZO

  4. 6.6 PROGRAMU ZA KIELELEZO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button