Kuhani Baraka: Kura yako ni nguvu yako, amani ndio nguzo ya taifa

MKUU wa Kanda ya Kusini wa Kanisa la Siloamu, Kuhani Baraka Zabwana Elia, ametoa wito kwa Watanzania wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29, akisisitiza kuwa kupiga kura ni wajibu wa kiraia na njia ya kudumisha amani na uongozi wa haki.

Amesema kura si tu kitendo cha kuchagua kiongozi, bali ni sauti ya wananchi inayotoa uhalali wa serikali na kuamua mustakabali wa taifa.

“Kupiga kura maana yake ni kushiriki katika utawala wa nchi yako. Bila kura yako, unaweza kutawaliwa na mtu usiyemtaka,” amesema.

Kuhani Baraka ameeleza kuwa msingi wa mamlaka yote upo mikononi mwa wananchi kama inavyobainishwa kwenye Ibara ya 8(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

“Kura ndiyo inayoleta uhalali wa utawala. Serikali hupata mamlaka yake kutoka kwa wananchi kupitia sanduku la kura,” amesema.

Akirejelea maandiko ya Biblia, ametaja Methali 18:18 inayoonesha kuwa “kura hukomesha mashindano,” akisisitiza kuwa kura ina nguvu ya kuamua hatima ya taifa.

Pia amenukuu Methali 29:2 akisema, “mwenye haki akitawala watu hufurahi, lakini muovu akitawala watu huangamia,” hivyo ni jukumu la kila mmoja kupiga kura ili kuleta uongozi wa haki.

Kuhani Baraka pia amewakumbusha waumini na wananchi wote kudumisha amani wakati wa uchaguzi, akisema amani ni nguzo ya maendeleo na msingi wa haki.

“Amani inaruhusu ustawi wa jamii, inatoa nafasi ya kupata haki na kuishi bila hofu. Ndiyo zawadi kubwa tuliyopewa na Mungu,” amesema akirejelea maneno ya Yesu katika Yohana 14:27, “Amani nawapa, si kama ulimwengu uwapavyo.”

Amewataka Watanzania wote kupiga kura kwa amani, bila jazba wala vurugu, akisema:

“Tuchague viongozi wenye moyo wa utumishi, kwa sababu kura sahihi inaleta amani na maendeleo, lakini kura isiyopigwa inaweza kumweka madarakani mtu asiyefaa.”

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I­ g­­­­­e­t­­­­ p­a­i­­­d­­­­­­­ o­­­­­v­e­r­ 2­­­2­­­0­­­ D­­­o­­­­­­lla­­­r­­­­­s p­­­­­e­­­­­r­ ­­­h­o­­­­­u­r­­­ ­­­­w­­­­o­r­k­­i­­­­n­g­ f­r­o­­m­ h­o­m­e­ ­w­i­t­h­­ 2 k­i­d­­s­ a­t­ h­o­­m­e­. i­ n­e­v­e­r­ t­h­o­u­g­h­t­ i­’d­ b­e­ a­b­l­e­ t­o­ d­o­ i­t­ b­u­t­ m­y­ b­e­s­t­ f­r­i­e­­n­d­ e­a­r­­n­s­ o­v­­e­r­ 1­5k­ a­ m­­o­n­t­h­ d­­o­i­n­g­ t­h­­i­s­ a­n­d­ s­­h­e­ c­o­n­v­i­n­c­­e­d­ m­e­ t­o­ t­r­­y­. it was all true and has totally ch­a­n­g­e­d­ ­m­y­ l­i­f­e­. T­h­i­s­­ ­i­s­ ­w­h­a­t­­ ­I­ ­d­­o­­­­­­­,­­­­­­­ ­c­h­­­­­e­­­­c­­­­k­ ­­­­i­­­­t­ ­o­­­­­u­t­ ­­­­b­y­ ­­­­V­i­s­­­­­i­t­i­n­­­­g ­F­o­­­­l­l­o­w­i­­n­­­­­g ­W­e­b­s­­­­­i­t­e

    ­
    Open This….  http://Www.Work99.Site

  2. I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
    Try it, you won’t regret it!….. https://www.Homeprofit1.site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button