Kundi la kwanza la wahamiaji lapelekwa Guantanamo Bay

MAREKANI : SERIKALI ya Marekani imetuma kundi la kwanza la wahamiaji katika kizuizi cha Guantanamo Bay, hatua inayokuja baada ya Rais Donald Trump kutangaza mipango ya kupanua kizuizi hicho.

Taarifa kutoka Idara ya Usalama wa Nchi zinasema kuwa wafungwa hao ni sehemu ya genge la Tren de Aragua, ambalo limetokana na magereza ya Venezuela. Wafungwa kumi walikusanywa kutoka kambi ya Jeshi la Fort Bliss, Texas, na kusafirishwa hadi kituo cha Jeshi la Wanamaji la Marekani kilichopo Cuba.

Wiki iliyopita, Trump alitangaza kuongeza uwezo wa kizuizi cha Guantanamo Bay ili kuhifadhi wahamiaji 30,000, kama sehemu ya juhudi za kudhibiti wahamiaji wasio na vibali nchini Marekani. Katika taarifa, Katibu wa Idara ya Usalama wa Nchi, Kristi Noem, alisema, “Rais Donald Trump amekuwa wazi, Guantanamo Bay itakuwa na wahamiaji wabaya zaidi.”

SOMA: Gereza la Guantanamo kupokea wahamiaji Elfu Thelathini

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button