Lengo ifikapo 2030 watalii mil 8

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kuelekea mwaka 2030 mpango wa serikali ni kukuza sekta ya utalii lengo likiwa kufikisha watalii wa ndani na nje milioni 8.

Amesema hayo wakati akifungua na kuhutubia Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bungeni mkoani Dodoma.

SOMA: Samia: Wizara maalum ya vijana kuanzishwa

“Tunaamini kwamba, kutokana na wingi na ubora wa vivutio pamoja na utajiri mkubwa wa kitamaduni, tunaweza kufikia lengo hili. Sasa ili kukuza utalii tutafungamanisha vivutio vya utalii ili mtalii atumie siku nyingi zaidi akiwa hapa nchini,.” amesema.

Samia amesema vyuo vya utalii na ukarimu vitaboreshwa, kwa kuongeza idadi ya watoa huduma wenye weledi katika fani zote za utalii na ukarimu sekta hiyoi nayo ni sehemu muhimu ya mpango wa kuzalisha ajira zaidi kwa wananchi na kuongeza akiba ya fedha za kigeni.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button