Leonardo: Simu ya mpenzi sio mali yangu

DAR-ES-SALAAM : MSANII maarufu wa vichekesho nchini Tanzania, Leonardo Datus, anayefahamika zaidi kwa jina la kisanii Leonardo, ameibua mjadala mkali mitandaoni baada ya kueleza wazi kuwa hawezi kushika wala kupekua simu ya mpenzi wake.

Leonardo amesema anathamini uhuru wa mtu binafsi na kwamba mapenzi yenye afya hujengwa katika misingi ya kuaminiana badala ya kudhibiti maisha ya mwenzi. “Kwanza kabisa, sichezeagi simu ya mpenzi wangu. Kwanini? Kwa sababu nina amani. Unajua mapenzi mazuri ni pale kila mtu anapokuwa na furaha yake binafsi,” alisema Leonardo kwa kujiamini.

Ameongeza kuwa chanzo kikuu cha migogoro mingi katika mahusiano ya kimapenzi ni tabia ya kushikiana simu, jambo linalochochea mashaka, chuki na kuondoa amani ya uhusiano. Hata hivyo, hoja hiyo imezungumzwa kwa mitazamo tofauti na baadhi ya mashabiki zake mitandaoni, Anna John, ameunga mkono kauli hiyo akibainisha uaminifu ndio msingi wa mahusiano bora .

Huku Ally Juma, akisisitiza kuwa mapenzi ya kweli yanapaswa kujengwa katika uwazi wa hali ya juu, na simu ni moja ya mambo yanayopaswa kushirikiana bila mipaka. Mjadala huu unaonesha namna suala la faragha dhidi ya uwazi katika mahusiano linavyobaki kuwa na mitazamo tofauti miongoni mwa jamii. SOMA:  Wachekeshaji waipamba ‘sendoff’ mtarajiwa wa Eliud

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button