Ligi mashuhuri kutangaza utalii wa Tanzania

DODOMA: LIGI za michezo mashuhuri duniani ni miongoni mwa maeneo yatakayotumika kutangaza utalii wa Tanzania katika mwaka wa fedha 2024/25. Bunge limeelezwa.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara yake mwaka wa Fedha 2024/2025.

“Kuendelea kutangaza utalii ndani na nje ya nchi ikiwa ni mwendelezo wa programu maalum ya Tanzania Th e R o y al Tour , filamu ya Amazing Tanzania pamoja na mikakati mingine mikubwa kupitia matangazo katika ligi kuu za michezo mashuhuri duniani.

“Matangazo kwenye ndege; misafara ya utangazaji utalii; matamasha makubwa ya kimataifa na mitandao mbalimbali ya kimataifa na vyombo vya habari,” amesema Waziri Kairuki.

Habari Zifananazo

Back to top button