Lishe duni ni changamoto kaskazini

ARUSHA: LICHA ya mikoa ya Kanda ya Kaskazini kuwa na utoshelevu wa chakula lakini bado kunachangamoto kubwa ya udumavu ,utapiamlo na lishe duni.

Kufuatia changamoto hiyo wataalamu wanatoa elimu nzuri ya kilimo na aina za vyakula vinavyopaswa kuliwa.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema hayo wakati akifungua Maonesho ya 31 Kilimo na Ufugaji Kanda ya Kaskazini, yanayoendelea kwenye viwanja vya Themi mkoani Arusha.

Amesema suala la lishe, udumavu na utapiamlo bado ni changamoto kubwa katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara na kuwataka wataalam wa lishe kutoa tathimini halisi ya changamoto hiyo sanjari na elimu zaidi kwa wananchi kula aina mbalimbali za vyakula vinavyostawishi miili.

“Msimu ujao wa maonesho hayo zitolewa tathmini ya hali ya udumavu na utapiamlo katika mikoa hii kwa changamoto ya lishe ni kubwa licha ya mikoa hiyo kusifika kwa uzalishaji wa chakula,” amesema Sendiga.

Ametoa rai kwa makatibu tawala wa mikoa ya kanda hiyo kufanya tathmini ya uwepo wa maonesho hayo ili kupima tija yake akihimiza umuhimu wa elimu zaidi kwa wakulima kutoka kwa wataalamu mbalimbali ikiwemo waoneshaji wa teknolojia na zana mbalimbali za kilimo badala ya kusubiri msimu wa nanenane pekee.

Humu akiwasihi wananchi kuchagua viongozi bora katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu nchini kwani uwepo wa viongozi bora wakiwemo madiwani na wabunge watawezesha maendeleo kupatikana kwa wakati na serikali kutatua changamoto zao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button