Lissu ajibu ‘makombora’ ya uchaguzi Chadema
DAR ES SALAAM; MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema ana sifa na uwezo wa kuongoza nafasi ya uenyekiti kwa weledi.
Lissu alisema kutokana na weledi wake kwenye uongozi, ndio maana Chadema ilimuona anafaa kugombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Shirika la Utangazaji la Uin gereza (BBC), Lissu alisema anashangazwa na maneno ya baadhi ya viongozi na wanachama wa Chadema wanaosema hafai kuongoza nafasi hiyo ya uenyekiti.
“Naambiwa na wanachama wangu na viongozi wenzangu kwamba huyu Lissu hafai kabisa, hafai hata kuongoza mtaa. Ila huyu Lissu ambaye hafai kabisa kuwa mwenyekiti alikuwa anafaa kuwa Rais kwenye uchaguzi wa mwaka 2020?” Alihoji.
Alisema hatishiki na maeno waliyombatiza baada ya kuingia kwenye mchuano wa kugombea uenyekiti kwa sababu anafahamu maneno hayo ni ya kiuchaguzi tu.
“Kutokukubalika hakunisumbui hata kidogo, kabla ya mwezi huu ambao nilisema ninagombea haku na mtu aliyekuwa ananiita mropokaji, nimeitwa majina mengi huu mwezi huu, nimeitwa majina mengi ambayo miezi mitatu iliyopita hayakuwepo kabisa,” alieleza Lissu ambaye mgombea mwingine wa nafasi hiyo ni Mwenyekiti wa sasa wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.
“Kwa sababu ni masuala ya uchaguzi unaelewa tu, kwa sababu uchaguzi unakuja na maneno mengi sana, unakuja na makelele mengi pia, hata wanaposema ninafaa kuwa mwan harakati na sio mwanasiasa ni maneno ya kiuchaguzi tu,” aliongeza Lissu.
Alisema katika majina anayoyakubali kati ya ma jina yote aliyobatizwa ni kuitwa mwanaharakati kwa sababu anaamini mwanaharakati ni mtu anayetetea maslahi ya wananchi kwa kiasi kikubwa, ambaye pia anaaminiwa na wananchi wanaomzunguka.
Alisema lengo la kugombea nafasi hiyo ni kutaka Mbowe astaafu kwa heshima kwa sababu tangu ashike nafasi hiyo miaka 21 iliyopita, amekijenga chama hicho vizuri.
“Kuna hatari moja sehemu ya kugombea kwangu ni kuhakikisha kwamba mwenyekiti analinda ‘legacy’ yake na kuokoa heshima aliyoijenga kwenye nchi hii,” alisema.
“Mwenyekiti Mbowe sisemi hajafanya kitu cha maana, amefanya kitu cha maana kwa kukitoa hiki chama kutoka wabunge watano, amekifanya kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania, mchango wake wa kihistoria kwa maende leo ya nchi hii utaan dikwa, nafasi yake katika siasa za Tanzania katika hii miaka 21 ya nafasi yake ipo salama,” alieleza Lissu.
Uchaguzi Mkuu wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa na viongozi wengine wakuu wa chama unatara jiwa kufanyika Januari 21, mwaka huu



