Luhemeja: Kianzishwe chombo cha fedha kuhifadhi Bioanuai
TANZANIA imesisitiza kuwa ili kuwa na uhakika wa fedha za hifadhi ya Bioanuai ni wakati muafaka sasa kuanzisha chombo maalumu chini ya Mkataba wa Hifadhi ya Bioanuai cha kuwezesha upatikanaji wa fedha za kuhifadhi Bioanuai kama ilivyoelekezwa katika Ibara ya 21 ya Mkataba huo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema hayo wakati akichangia hoja katika majadiliano yanayoendelea katika sehemu ya pili ya Mkutano wa 16 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Hifadhi ya Bioanuai yanayofanyika Roma, Italia.
Sambamba na hilo, Tanzania imesisitiza kuwa ni vyema pia kufanya tathmini ya mifuno ya fedha iliyopo ili kuiimarisha katika kuwezesha masuala ya uhifadhi wa Bioanuai Duniani.



