Lukuvi asihi vijana kuwa uelewa wa mazingira

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) William Lukuvi ametoa wito kwa vijana kuendelea kujijengea uwezo ili kuwa na uelewa kuhusu mazingira.
Ametoa wito huo alipokutana na vijana wa kitanzania wanaojihusisha na masuala ya mazingira jijini Nairobi, Kenya unakofanyika Mkutano wa Saba wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-7).
SOMA: Tanzania yasihi dunia kukabili changamoto za mazingira
Lukuvi amewasihi vijana hao kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika katika ulinzi na uhifadhi wa mazingira kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo upandaji wa miti.
Ameongeza kuwa vijana ni nguvu kazi muhimu katika taifa hivyo hawana budi kushirikiana kwa pamoja kulisaidia taifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na hiifadhi ya mazingira kwa ujumla.
Lukuvi amesema kuwa kutokana na umuhimu wao, Serikali itawapa nafasi vijana katika kushiriki na kutoa mchango wao katika masuala ya mazingira.
Katika kikao hicho, vijana wameishukuru Serikali kwa kuwapa nafasi za kushiriki katika Mkutano huo wa UNEA-7 pia kuendelea kuwajengea uwezo na kushirikiana nao kwa maendeleo ya nchi.




Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com