MA-DC wapya wapewa vipaumbele

TANGA: UKUSANYAJI mapato, usimamizi wa miradi ya maendeleo, uwekezaji, utatuzi wa migogoro ya ardhi sambamba na kuimarisha kilimo cha mazao ya biashara ni vipaumbele vitano ambayo wameelezwa wakuu wa wa wilaya wapya wa Mkoa wa Tanga.
Vipaumbele hivyo vimetajwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batlida Burian wakati wa zoezi la kuwaapisha viongozi hao wawili lililofanyika leo Juni 30, 2025 jijini humo.

Batlida amesema imani yake ni kuwa viongozi hao watakuwa sehemu ya mabadiliko kwa wananchi kwenye maeneo yao na mkoa kwa ujumla.
“Nendeni mkailinde na kuitunza imani ya Rais lakini tunategemea ubunifu mkubwa katika maeneo ya viumbele ili kuweza kutimiza lengo la kumletea maendeleo mwananchi,”amesema.




