Maafisa utamaduni, michezo wamefikiwa mambo ya kisasa TSN

DAR ES SALAAM; KIKAO kazi cha maafisa utamaduni pamoja na mafisa michezo kimeendelea ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na leo wamepewa somo namna ya kusoma mtandaoni magazeti ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).
TSN ni wachapishaji wa magazeti ya DAILY NEWS, HabariLEO na SpotiLeo, pia ina mitandao ya instagram, facebook na x kwa magazeti hayo, pamoja na chaneli ya Daily News Digital na tovuti rasmi za magazeti hayo.
Kaimu Meneja wa Huduma za Habari za Kidijiti wa TSN, Sylivestre Domasa akiwasilisha mada kwenye kikao kazi hicho, amesema kuna mfumo wa E-Paper ambao ni rahisi kuweza kusoma magazeti ya kampuni hayo, kwani dunia kwa sasa dunia ni kama kijiji, kila kitu kinapatikana mtandaoni.
“Unaweza kupakua na kusoma habari kutoka magazeti ya Daily News, HabariLEO na SpotiLEO kupitia mtandao wa E-Paper kwa gharama nafuu na kwa haraka zaidi,” amesema Domasa.
Amefafanua kuwa mtu anachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye mtandao na kulipia kwa bei nafuu ili kupata toleo la gazeti, ikilinganishwa na gharama ya gazeti la kawaida.
Amesema kupitia mfumo huo, msomaji anaweza kupata leo habari zilizopo kwenye gazeti la kesho, kwani taarifa hizo hupatikana mtandaoni mapema kwa waliolipia huduma hiyo..
penis enlargement
If you would like to obtain a good deal from this paragraph then you have to apply these
methods to your won web site.