Mabondia kuchapana Nov.30

JUMLA ya mabondia 30 wamepima afya tayari kwa maandalizi ya mwisho kuelekea pambano la ‘Dar Boxing Derby’ linalotarajia kupigwa Novemba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam.

Miongoni mwa watakaocheza mapambana hayo ni Ally Ngwando wa Manzese ambaye anatarajia kucheza pambano kuu ‘main card; dhidi ya Ismail Boyka kutoka Gongo la Mboto, Dar es Salaam huku kiingilio katika pambano hilo kikiwa ni Shillingi 5000 na Shillingi 10,000 mlangoni na Shillingi 15000 VIP.

Mratibu wa pambano hilo, Bakari Khatibu amesema kuwa wamekamilisha zoezi la kwanza kwa upimaji afya za mabondia kuelekea kwenye pambano hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo huo.

“Tayari leo  tukiwa kama waandaji tumekamilisha sehemu ya kwanza ya maandalizi kwa kuwapima afya mabondia wote kutokana na kanuni na sheria za mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini.”Amesema Khatibu na kuongeza

“Kitu kikubwa ambacho tunataka kuwaambia mashabiki tukiwa kama waandaji tumekuwa tukifanya mambo kwa utofauti mkubwa kwa sababu wasitegemee kuona Uwanja wa Kinesi kuwa unavyokuwa kwenye mapambano mengine, tumejipanga kuleta utofauti na hata wale ambao watakuwa wamekata tiketi za VIP basi watapata hadhi ya kuwa katika VIP,” amesema Khatibu.

Miongoni mwa mabondia waliopima afya ni Karimu Mandonga ambaye amewataka mashabiki wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi katika pambano hilo la ‘Dar Boxing Derby’ huku akisisitiza kuwepo kwa ngumi yake ya ndoinge kwenye pambano hilo.

“Tayari tumekamilisha zoezi la kupima afya kwa ajili ya maandalizi ya pambano la Dar Boxing Derby na jambo kuwa ni kuhamasisha wadogo zetu hiyo siku mashabiki wanataka kushuhudia ngumi hasa yaani watu wapigane mpaka Yesu azaliwe tena na ngumi ndoige zionyeshwe,”.

Mabondia wengine watakaopanda ulingoni kwenye pambano hilo ni Gilbert Machupa dhidi ya Juma Kichupa, Joseph Maigwisa na Ibrahim Tamba lakini Mudy Pesa akitarajia kucheza na Man Chuga huku Yuko Kyando akipewa kucheza na Hemedi Rashid.W

engine ni Vigulo Shafii na Bakari Dunda, Hamad Furahisha dhidi ya Max Mushi, Paul Magesta na Haruna Ndaro, Emmanuel Kitimtim na Swahibu Ramadhan wakati Mshamu Mohamed atacheza na James Killian huku Peter Tosh akipewa kuzima na Jackson Malinyingi.

Habari Zifananazo

Back to top button