Mabula amshukuru Rais Samia Sh bilioni 4 sekta ya kilimo

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dk Angelina Mabula amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wilaya ya Ilemela Sh Bilioni 4.6 katika Sekta ya Ardhi kwaajili ya kupanga na kupima viwanja lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia ardhi yao .

Dk Mabula amesema hayo leo Machi 31, 2023  wakati wa ziara yake katika Kata ya Nyasaka viwanja vya Mkombozi .

“Katika kipindi chake cha miaka miwili Rais Mhe Samia ametutendea makubwa sana, Tumshukuru na tuendelee kumuombea kwani Ilemela tumepewa fedha nyingi za maendeleo.” Alisema

Dk  Mabula amewataka Vijana kuchangamkia mikopo inayotolewa na Halmashauri ili waweze kujikwamua kiuchumi lakini pia alitumia hadhara hiyo kukemea vitendo vya ulawiti pamoja na mapenzi ya jinsia moja pamoja na vitendo vya unyanyasaji na ukatili vinavyoendelea katika jamii huku akiwataka wananchi kuripoti polisi vitendo hivyo vinapojitokeza.

Waziri Mabula yupo ziara jimboni kwake kwaajili ya kukagua miradi mbalimbali pamoja na kuhamasisha shughuli za maendeleo.

Habari Zifananazo

Back to top button