Machumu ateuliwa Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amemteua Bakari Steven Machumu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, akichukua nafasi ya Sharifa Nyanga ambaye amepangiwa majukumu mengine ya Serikali.

Uteuzi huo unaweka sura mpya katika mfumo wa mawasiliano ya Serikali, ukitarajiwa kuongeza uimara wa utoaji wa taarifa za Serikali kwa wananchi na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi. SOMA: UTEUZI: Kabudi apewa Wizara ya Michezo, Silaa Mawasiliano

Machumu, ambaye ni miongoni mwa wataalamu wenye uzoefu mkubwa katika tasnia ya habari na mawasiliano, ameongoza sekta ya vyombo vya habari kwa zaidi ya miaka 20, akifanya kazi katika nafasi za juu za uhariri na uongozi, ikiwemo Mwananchi Communications Ltd (MCL).

Uteuzi wake unaelezwa kuwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuimarisha mikakati ya mawasiliano na kuibua taswira chanya ya Taifa katika zama za uenezaji wa habari wa kidigitali.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button