RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Mosses Kusiluka imefafanua kuwa Rais Samia amemteua Jerry Silaa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Aidha, katika taarifa hiyo ya uteuzi, Rais Samia Damas Ndumbaru kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Awali alikuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo.
Mhandishi Hamad Yusuf Masauni ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais( Muungano na Mazingira)
Hata hivyo, Ashatu Kijaji ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Abdallah Ulega ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi, awali Ulega alikuwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo.
Inocent Bashungwa ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.