Madhara ya ukosefu wa amani kwa wanafunzi kitaaluma

JUZI gazeti hili liliandika makala chini ya kichwa cha habari: ‘Vijana Vyuoni na Tanzania Yenye Utajiri wa Amani’ yakieleza maoni ya vijana wanaoendelea na waliohitimu masomo yao katika vyuo vikuu nchini kuhusu ukosefu wa amani unavyoweza kuathiri masomo yao kitaaluma.
Leo katika makala haya, anaendelea kubainisha namna vijana hao kuhusu faida za mujenga, kutunza na kudumisha amani sambamba na hasara za kuchezea na hatimaye kupoteza tunu ya amani. ENDELEA… AMANI ni msingi muhimu katika mazingira ya elimu, hasa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaohitaji utulivu wa kimwili, kiakili na kijamii ili wajikite katika masomo yao.
Kukosekana kwa amani, kunakoweza kusababishwa na machafuko ya kisiasa, vurugu za kijamii, migogoro ya kikabila, vitisho vya usalama, au hata hali ya kulazimika kuhama, huathiri kwa kiasi kikubwa ustawi wa wanafunzi na hatimaye ufanisi wao kitaaluma.
Hii ni kwa kuwa katika mazingira yasiyo na amani, wanafunzi hupatwa na msongo wa mawazo, wasiwasi au hata mshituko wa kiakili. Hisia hizo hupunguza uwezo wao wa kuzingatia masomo, kukariri taarifa, kujadili, kutafakari, kuelewa na kufanya mitihani kwa kujiamini.
Badala ya kuelekeza akili kwenye masomo, nguvu nyingi hutumika kufikiria juu ya usalama wao na wa familia zao. Mwanafunzi wa uhandisi mitambo katika Chuo cha Ufundi Arusha, Joseph Makasi anasema kukosekana kwa amani kumesababisha kuharibika kwa ratiba ya kufungua chuo.
Anasema wakati na hata baada ya uchaguzi zilitokea vurugu zilizosababisha vyuo na vyuo vikuu kuchelewa kufunguliwa jambo lililowasabisha kuchelewa kuanza muhula mpya wa masomo. “Pia, tunakosa kuwa na usikivu na ufuatiliaji mzuri wa masomo darasani na katika muda wa ziada kwa kuwa hofu inatutawala muda wote, unahisi lolote linaweza kutokea wakati wowote,” anasema Makasi.
Madhara mengine yanatokana na ukweli kuwa mara nyingi machafuko au ukosefu wa amani husababisha kusimamishwa kwa shughuli za kitaaluma. Kufungwa kwa vyuo, kutokufanyika kwa mihadhara, au kutoweza kuhudhuria kwa sababu za usalama kunapunguza muda wa kujifunza.

Hii huathiri utaratibu na mwendelezo wa kozi, na kuwafanya wanafunzi washindwe kufuata ratiba ya masomo kama ilivyopangwa. Mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Ndaki ya Karume, Zanzibar kozi ya Usimamizi wa Maendeleo ya Jamii, Naomi Msigwa: “Kukosekana kwa amani kunaathiri ratiba zetu za kitaaluma, kama ambavyo sasa vyuo vimechelewa kufunguliwa, kuna ratiba kama za ‘research’ (utafiti) au ‘projects’ (miradi) pia zimechelewa kutokana na hilo.”
Wadau wanasema katika eneo lenye vurugu, miundombinu hudhoofika, maktaba kufungwa, huduma za mtandao kukatika, au vifaa muhimu kuharibika. Hata wanafunzi wanaotegemea kujifunza kwa kutumia mtandao hukumbana na kikwazo cha miundombinu isiyo imara.
Matokeo yake, uwezo wa kufanya utafiti au kuandaa kazi za kitaaluma hupungua. Naye Muzdat Mussa ambaye mwanafunzi wa Shahada ya Mawasiliano kwa Umma, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) naye anazungumzia sauala hilo. Anasema: “Kukosekana kwa amani kutapunguza uwekezaji katika miundombinu ya elimu, serikali na wadau wengine watakosa uwezo wa kuwekeza katika miundombinu ya shule inayohitajika ili kutoa mazingira bora ya kusomea.”
“Hali hiyo inapelekea shule nyingi kuwa na vifaa duni na mazingira yasiyofaa kwa wanafunzi na kuathiri moja kwa moja utendaji wao kitaaluma,” alisema. Wadau mbalimbali wa amani wanasema tunu hiyo ikikosekana huathiri uchumi wa familia hali ambayo kwa namna moja ama nyingine huathiri pia masomo ya wanafunzi ama wawe wa elimu ya msingi, vyuo au vyuo vikuu. Kwa mujibu wa uchunguzi wa HabariLEO, wazazi au walezi wanaweza kupoteza ajira au mali, jambo linaloathiri vibaya uwezo wao kugharamia ada, chakula, na makazi ya wanafunzi.

Madhara mengine ya hali hiyo yanaweza kuwa baadhi ya wanafunzi kulazimika kufanya kazi kwa muda ili kujikimu, hivyo kupunguza muda wao wa kujifunza ama iwe darasani au katika muda wa ziada nje ya muda wa darasa.
Suala hilo linaungwa mkono na hoja ya Mwanafunzi wa Shahada ya Uhasibu na Fedha katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, Abubakar Shaaban Khalfan Abubakar ukosefu wa amani husababisha changamoto za kiuchumi katika familia kwa kuwa amani inapokosekana, wazazi wengi hupoteza ajira au kipato, hivyo kushindwa kulipia ada, vitabu au mahitaji ya mwanafunzi. “Wanafunzi hulazimika wakati mwingine kutafuta kazi ndogondogo ili kusaidia familia, hivyo kukosa muda wa masomo,” anasema Abubakar.
Mwanafunzi wa Shahada ya Utawala wa Umma, SUZA, Huzaima Malik anasema: “Kukosekana kwa amani husababisha wazazi kushindwa kumudu gharama mbalimbali za elimu kama ada na mahitaji mengine ya kitaaluma kwa kuwa wazazi watashindwa kufanya shughuli za uzalishaji.” SOMA: Askofu awasihi vijana kudai haki kwa kuzingatia amani
“Hiyo nayo husababisha wanafunzi kukatisha masomo wakati mwingine,” alisema. Naomi Msigwa wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Zanzibar anasema kiuchumi wazazi wengi ni wale wa kutoka kila siku kwenda kazini au kwenye biashara zao ili familia zipata mahitaji ya kila siku ili ziweze kuishi na wasipotoka, tatizo lingine linaongezeka la kukosa hata chakula.

Kukosekana kwa amani kunawasababisha washindwe kutafuta mahitaji ya familia. Kwa upande wake, Altourab Haji wa Taasisi ya Utawala wa Umma Zanzibar (IPA) anasema kukoseakana kwa amani husababisha kukosekana kwa mazingira salama ya kujifunzia.
Aidha, anasema kukosekana huko kunaweza kutokea kwa uharibifu wa miundombinu ya elimu yote inayohusisha elimu kama vile majengo mbalimbali ikiwemo madarasa na maktaba na huleta msongo wa mawazo na changamoto za kisaikolojia.
Kuhusu suala hilo, Muzdat wa SUZA anasema: “Kukosekana kwa amani kutapunguza uwekezaji katika miundombinu ya elimu; serikali na wadau wengine watakosa uwezo wa kuwekeza katika miundombinu ya shule inayohitajika ili kutoa mazingira bora ya kusomea.”“Hali hiyo inapelekea shule nyingi kuwa na vifaa duni na mazingira yasiyofaa kwa wanafunzi na hapo moja kwa moja kuathiri utendaji wao wa kitaaluma.”
Mwanafunzi wa Shahada ya Uhasibu na Fedha katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, Abubakar Shaaban Khalfan anasema amani inapokosekana husababisha kwenda nje ya ratiba kimasomo ambapo inawapa kazi kubwa walimu kwenye kumaliza ‘syllabus’ (mwongozo wa masomo) na kulazimisha wanafunzi kusoma vitu vingi kwa mda mdogo “Uharibifu wa rasilimali za kimasomo kama majengo, hupunguza uwezo wa kujifunza,” anasema.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com