Madiwani Mikindani watakiwa kusimamia ukusanyaji mapato

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara wametakiwa kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika manispaa hiyo.

Akizungumza mkoani Mtwara wakati wa kikoa cha Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo kuhusu kupitia taarifa mbalimbali za robo ya pili kwa mwaka fedha 2024/2025 kilichofanyaika kwenye manaspaa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Abdallah Mwaipaya amesema ukusanyaji wa mapato ndiyo uti wa mgongo wa manispaa hiyo.

Advertisement

‘’Kazi ya halmashauri ya manispaa kubwa mbili za msingi ni ukusanyaji wa mapato lakini pia usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo hizo ndiyo shughuli kubwa ambazo manispaa na halmashauri nyingine yoyote mnapaswa kuzisimamia lakini kuna suala la usimamizi wa utawala bora’’amesema Mwaipaya.

Aidha ameipongeza manispaa hiyo kwa kufanya vizuri kwenye suala la ukusanyaji wa mapato katika wilaya hiyo ya mtwara kwa kuwa ndiyo inayoongoza kwa kutoa fedha nyingi kwenda kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa na manispaa kupitia mapato yake ya ndani.

Licha ya manispaa hiyo kufanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa miradi lakini bado kuna baadhi ya miradi ambayo bado inaendelea na haijakamilika hivyo waendelee kuweka nguvu kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kwasababu wananchi wanahitaji kuona miradi inakamilika na waweze kupata huduma.

Ofisa Usimamizi Fedha Mkoa wa Mtwara, CPA Norbert Shee amesema manispaa hiyo inaendelea vizuri kwenye utekelezaji wa miradi na mingi imesimamiwa vizuri na kuiona thamani ya fedha na kuutaka uongozi wa manispaa kuepuka suala la urasimu ili wasije wakakwama katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Meya wa Manispaa hiyo, Shadida Ndile amewasisitiza madiwani na uongozi wa manispaa kwa ujumla kuwa, wanapopewa pongezi hizo wasirudi nyuma na badala yake waongeze kasi kuhakikisha wanaendelea kukusanya fedha kadri wanavyoweza lakini miradi inayotekelezwa wahakikishe inakuwa ya kiwango kinachotakiwa.

Baadhi ya madiwani hao akiwemo Diwani wa Kata ya Magomeni, Lameck Mlaponi amesema watazingatia maagizo yote yaliyotelewa kwenye kikoa hicho hasa suala lau tekelezaji wa miradi mbalimbali katika kata zao.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *