TANGA: BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Tanga limepitisha Rasimu ya Bajeti ya Sh bilioni 83.3 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 huku Sh bilion 10.2 ya fedha hizo zikitengwa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Rasimu ya bajeti hiyo imepitishwa leo wakati wa mkutano maalumu wa baraza hilo, ambapo halmashauri hiyo imepanga kukusanya Sh bilioni 25 katika vyanzo vya mapato ya ndani vya mapato.
Akiwasilisha mapendekezo ya bajeti, Kaimu Mchumi wa Jiji la Tanga, Juma Mkombozi amesema wanatarajia kupata fedha hizo kutoka katika vyanzo vya ndani, ruzuku ya serikali pamoja na wahisani mbalimbali wa maendeleo.
Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurahman Shiloo amesema kuwa rasimu hiyo ya bajeti inakwenda kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato na hivyo kusaidia utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo.
Alisema vipaumbele kwenye bajeti hiyo ni pamoja na kukamilisha miradi viporo ikiwemo ya elimu na afya, kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato na kupunguza mianya ya upotevu wa mapato.
“Tuwekeze nguvu ya kutosha kwa maarifa na ubunifu wetu wote katika usimamizi wa ukusanyaji na matumizi ya mapato ya halmashauri, kwasababu changamoto zote zinahitaji fedha na mapato ndiyo yatatufanya tuwahudumie wananchi, ” amesema Meya huyo.
It’s appropriate time to make some plans for the future and it is time to be
happy. I have read this post and if I could I wish to suggest you few interesting
things or suggestions. Maybe you could write next articles referring to this article.
I desire to read more things about it!