Mafia Boxing wagawa mitungi kwa wajasiriamali

DAR ES SALAAM; KAMPUNI ya Mafia boxing Promotion imegawa majiko ya gesi kwa mama lishe wa Magomeni Sokoni, ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa Samia Suluhu Hassan kuondokana matumizi ya nishati ya mkaa.

Mama lishe hao zaidi ya 30, wamepatiwa majiko wakati wa kuwatambulisha mabondia 14 watakaopanda ulingoni leo kwenye KnockOut ya Mama.

Akizungumza baada ya kugawa majiko hayo Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion, Ally Zayumba, amesema wameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha wanaunga mkono harakati za Rais Samia za kuondokana na matumizi ya nishati chafu kwa Watanzania.

“Rais wetu, Dk Samia amekuwa akihamasisha Watanzania kuachana na matumizi ya nishati chafu ambayo ni mkaa na kuni, nasi tukaona hatuna budi kuunga mkono jitihada hizo kwa kugawa majiko kwa Mama lishe wenye mahitaji katika soko hili la Magomeni,” amesema.

Zayumba alizindua makala maalumu na kuonesha wananchi namna Rais Samia alivyokuwa msaada kwenye sekta mbalimbali ikiwemo kuinua michezo bila kubagua na kumshukuru kwa kuwa pamoja nao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button