JAJI wa Mahakama Kuu anayesikiliza kesi ya Mbunge wa Viti Maalum Halima Mdee na wenzake 18, Jaji Cyprian Mkeha amesema atatoa uamuzi Septemba 2, 2022 ikiwa makada hao wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) watahojiwa wakiwa mahakamani au la.
Mawakili wa Mdee na wenzake wamepinga mahakama kuruhusu wateja wao kuhojiwa kwa kuwa wao ndio wanaoshitaki na kwamba upande unaopaswa kuwahoji ni wa washitakiwa (Chadema).
Jaji Mkeha amesema atatoa uamuzi saa nane na nusu mchana iwapo Mdee na wenzake watatakiwa kuhojiwa na kwamba kwa sasa hawapaswi kufika mahakamani siku hiyo ya uamuzi.
Mdee na wenzake saba wamefika Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza tangu wafungue shauri hilo baada ya kutakiwa kufanya hivyo ili waweze kuhojiwa. Hata hivyo, Jopo la mawakili linalo watetea wamepinga hatua hiyo ambayo sasa itatolewa uamuzi Septemba 2.