Mahakama yamhukumu Luwongo kunyongwa

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam iliyoketi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mfanyabiashara, Khamis Luwonga ,38, kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya aliyekuwa mke wake Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa.
Hukumu hiyo ilitolewa leo na Jaji Hamidu Mwanga na kabla ya kutoa adhabu hiyo alitoa maelezo yaliyopelekea mshitakiwa kukutwa na hatia katika kosa hilo.
Awali Jaji Mwanga alisema mshitakiwa alitia hatiani kwa kosa hilo kutokana na ushahidi uliotolewa na mashihidi 14 pamoja na vielezo kikiwemo melezo ya onyo ambayo mshitakiwa alichukuliwa akiwa katika kituo cha polisi.
Jaji Mwanga alisema kuwa katika ushahidi uliotolewa ilidaiwa kuwa kulikuwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya Khamisi na mkewe Naomi na baadaye marehemu alidaiwa kupotea, katika kupotea huko Khamisi alitoa taarifa za kutoonekana kwa mke wake ikiwemo katika vituo vya polisi.
Akiwa anaendelea kufuatilia taarifa za mke wake Khamisi alidai kuwa alitumiwa ujumbe kutoka kwa Naomi akimwambia kuwa aliamua kwenda nje ya nchi hivyo alimtaka awe analea mtoto wao.
Ilidaiwa kuwa Julai 16,2019 katika kituo cha polisi cha kati wakati Khamisi akiwa anaendelea na harakati za kutoa taarifa polisi juu ya maendeleo ya mke wake alihojiwa kuhusu jumbe alizodaiwa kutumiwa na mke wake kwani kwa uchunguzi wa kielektroniki ilionyedha kuwa jumbe hizo zilitumwa katika sehemu moja.
Aidh, Jaji alisema ni jukumu la upande wa mashitaka kuthibitisha hatia ya mshitakiwa na katika mauaji inatakiwa kuthibitishwa kama mtu kweli amekufa na kifo chake kuwa sio cha kawaida.
Alisema katika kesi kuna mazingira tofauti kidogo na mazingira yake yanaonyesha kuwa hakukuwa na mwili kuthibitisha kuwa kweli Naomi amekufa na kama hakuna mwili basi uchunguzi wa kitabibu haukufanyika kubaini marehemu alikufa kwa sabbau au kutokana na nini.
Aliongeza kuwa kutokana na kesi zilizothibitishwa kutoka nchini India zilionyedha kuwa kufo cha mtu kinaweza kuthibitishwa kwa ushahidi wa mazingira ambayo kifo hicho kimetokea na uchunguzi unaweza kufanya pasipokuwa na mwili.
“Sio lazima kuwe na mwili ikiwa ni suala la lazima kuwepo na mwili ili kuthibitisha hatia tutawapa na watu upenyo wa kuteketeza ili kukimbia ushahidi,” alisema Jaji Mwanga.
Pia alisema kuwa katika mashahidi hao wapo waliokwenda Morogoro na kwa upande wa mkemia alileta majibu kuwa alishindwa majibu ya moja kwa moja kwani ilibainika mabaki yaliyopatikana yalikuwa ni ya mmwanamke lakini haikuthibitihshwa kuwa ni ya Naomi .
Jaji Mwanga alisema kuwa katika maelezo ya onyo ya Hamisi alidai kuwa mabaki yale ni ya ya Naomi na alidaiwa kuwa Naomi amefariki na mshitakiwa ndiyo aliyemuua na pia chumba alichokuwa akilala Naomi kilikutwa na mabaki ya damu na yalidaiwa kuwa ni ya Naomi.
Pia kwa mujibu wa maelezo ya onyo ya mshitakiwa alidai kuwa Mei 14,2019 ni siku ambayo hakulala nyumbani kwake kwani alilala kwa Margreth alirudi kwake asubuhi na kumkuta mke wake akimuandaa mtoto kwenda shule alidai alimpita bila kusema chochote na mtoto alichukuliwa na bodaboda kupelekwa shule.
Aliendelea kudai kuwa simu iliita kwa jina la Magreth ndipo Naomi alianza Kumtukana na Hamisi akamwambia achukue chochote anachokitaka kwani hakukuwa na ndoa tena kati yao wakati wa ugomvi Naomi alidondoka chini na kujigonga kichwani na damu zikaanza kutoka akawa analalamika akitetemeka sitomsamehe.
Baadaye alianza kukoroma hadi umauti ulipomfika baada ya Naomi kufa Hamisi akataka kuundoa mwili ndipo alipouzungusha kwenye shuka mbili na baada ya kuona kuwa akitoka na mwili ule kwenye gari akiwa barabarani askari wangemsimamisha na kuuona ndipo alipokumbuka katika banda la kuku kulikuwa na shimo kwa anili ya kupitisha maji.
Alipokumbuka hili alichukua mwili na kwenda kuuchoma na magunia mawili ya mkaa ili uungue taratibu kwani alihofia kuchoma na kuni zingekuwa nyingi na wakati mwili ulipoungua na kubaki mkaa alimtuma bodaboda kwenda kununua mafuta na alipofiki alikwenda kuyachukulia getini ili asiingie ndani.
Pia jaji aliendelea kusema kuwa maelezo hayo yanaeleza kuwa kwakuwa mafuta ya taa yangeisha haraka akachukua viatu na kuviweka ili uendelee kuungua taratibu na baada ya hapo alichukua mabaki na majibu na kupanda gari yake aina ya Subaru na kuondoka hadi shambani kwake Morogoro ndipo alipofukia na kupanda Mgomba juu ya mabaki hayo.
Jaji alisema hakuna mtu anayeweza kutoa mtiririko huo wa matukio isipokuwa tule anayejua ukweli wa tukio hilolilivyotolea, hivyo alisema kuwa maelezo hayo ni ya kweli na ya kuaminika.
Pia alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mashihidi namba nne ambaye alikuwa ni Mpwa wake ni wa kuaminika kwani hakuwa na sababu ya kumuongelea uongo mjomba wani kwa sababu ndiye aliyemtoa kijijini kumleta Dar es salaam kwa ajili ya kufanya kazi.
Baada ya mshitakiwa kutkutw ana hatia alipata nafasi ya kujitetea na katika utetezi wake alidai kuwa maelezo hayo ya onyo yalikuwa si ya kwake na jaji alisema mahakama ilitupilia mbaki kwani hakukataa maelezo hayo mara ya kwanza yalipoletwa kama kilelezo mahakamani.
Alisema pia mahakama inaangalia baada ya mauaji ni kutu gani kilitendeka na kwa mujibu wa maelezo maada ya mauaji aliviringisha mwili kwenye shuka mbili na kwenda kuuchoma na kwa mujibu wa maelezo hayo inaonyesha mshitakiwa alidhamiria kutenda kosa.
Pia mawakili wa mshitakiwa walidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa akiwa hana akili timamu na alichukuliwa na kupimwa uwezo wake wa kufikiri lakini kutokana na mtiririrko ulivyojieleza mshitakiwa alionekana kuwa na akili timamu kwani aliweza kufikiria kutenda matukio yote.
Jaji alisema kuwa mahakama hiyo ilimtia hatiani mshitakiwa kwa kumuua mke wake chini ya kifungu namba 196 na 197 cha sheria ya adhabu.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ashura Mzava alieleza mahakama kuwa mshitakiwa hana rekodi ya makosa ya nyuma lakini aliiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe funzo kw awanaume wote kwani kifo cha Naomi kimeonyesha kuambatana na mateso makali na kufanya vijana na watu wengine kuwa na hofu kuingia katika ndoa.
Pia aliiomba mahakama ikabidhi kielelezo namba PW8 ambacho ni mabaki wa mwili wa Naomi kwa familia yake ili aweze kupewa heshima ya mwisho ya kidini ambayo hakupewa baada ya kifo chake.
Baada ya kuelezwa hayo jaji alisema kuna adhabu moja tu kwa kosa la mauaji na kwakiwa mshitakiwa amekutwa na hatia kwa kosa hilo mahakama imemuhukumu kunyongwa mpaka kufa.



