Majaliwa: Serikali iungwe mkono huduma za jamii

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewasihi viongozi wa taasisi za dini waendelee kuiunga mkono serikali katika utoaji wa huduma za jamii hasa kipindi hiki ambacho imewekeza katika miundombinu ya afya, elimu na maji.

Majaliwa alisema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za dini kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora, nafuu na kwa wakati katika maeneo yao. Alisema hayo jana Ngaramtoni, Arusha wakati wa ibada ya kusimikwa kwa Askofu wa Kanisa la Baptist Tanzania, Arnold Manase Mollel na viongozi waandamizi.

“Ninapenda niwahakikishie kwamba Serikali kwa upande wake imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu, afya na maji katika kuhakikisha watanzania wote bila kujali dini zao, rangi zao au itikadi zao wanahudumiwa ipasavyo”alisema Majaliwa.

Alitoa mfano wa sekta ya afya, Majaliwa alisema serikali imeongeza fedha za kusomesha wataalamu bingwa na bobezi katika sekta ya afya hadi kufikia shilingi bilioni 8 kutoka shilingi bilioni 3 za mwaka wa fedha 2021/2022.

“Hii itasaidia kuboresha huduma kwa wananchi na kupunguza rufaa za nje ya nchi” alisema.

Aidha, Majaliwa alizipongeza taasisi za dini ikiwemo kanisa la Wabaptist wa Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwaongoza watu na kutatua shida zao za kijamii, kuwapa mafundisho ya kiroho, kutoa ushauri na kuwajenga kiimani.

“Kwa mfano, katika jumla ya shule za Msingi 19,261 zilizopo nchini, sekta binafsi na taasisi za dini zinamiliki shule zipatazo 2,080. Kwa upande wa Shule za Sekondari 5,540, shule 1,329 ni za Sekta Binafsi na Taasisi za Dini” Kadhalika Majaliwa amempongeza Baba askofu Anorld Manase Mollel kwa kusimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Wabaptist.

“Kusimikwa kwako leo ni ishara ya wazi kuwa waumini wa Kanisa la Wabaptist Tanzania wanayo imani kubwa na wewe na ndiyo maana wamekupa nafasi hiyo ili uweze kusimamia maono na malengo ya ya Wabaptist wa Tanzania.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x