Majaliwa: Tanzania ni mahali sahihi kuwekeza

DODOMA; WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema serikali imerekebisha changamoto ambazo wawekezaji wengi walikuwa wakizilalamikia, ili kufungua milango wawekezaji wengi kuja kuwekeza kwani Tanzania ni mahali sahihi pa kuwekeza.

Ametoa kauli hiyo leo bungeni, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ushetu, Emmanuel Cherehani aliyehoji mkakati wa serikali kuhusu viwanda mbalimbali ikiwemo pamba, tumbaku na korosho.

“Nataka niwahakikishie wawekezaji wote kuja Tanzania kuwekeza kwa sababu Tanzania ni nchi iliyobahatika imekaa kimkakati zaidi, ina nchi nane jirani zinategemea soko la Tanzania.

“Tanzania ipo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ina idadi kubwa ya wateja, Tanzania ipo kwenye Jumuiya ya SADC, zina idadi kubwa ya wananchi wanaotegemea soko la Tanzania. Uwepo wa Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, “amesema Waziri Mkuu na kuongeza kuwa Tanzania ni mahali sahihi pa uwekezaji.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button