Majirani wazuia jeneza la kijana kuingia kwa wazazi

WANANCHI wa Mtaa wa Magan[1]ga, maeneo ya Nurulyakini, Temeke, Dar es Salaam wamezuia mwili wa marehemu Pius Beda maaru[1]fu Stahimili (32) kuingia nyumbani kwa wazazi wake, kuonesha hasira zao kwam[1]ba wazazi hao walishindwa kumhudumia alipokuwa hai.

Kijana huyo alikutwa amekufa kwa kujinyonga nyumbani kwa ji[1]rani alikokuwa anasaidiwa mahala pa kulala.

Wakizungumzia mkasa huo Dar es Salaam jana, majirani wa Stahimili walisema amekuwa akii[1]shi maisha magumu kiasi kwamba hata alipotafuta msaada kwa baba na mama yake wa kambo alio[1]kuwa anaishi nao hakusaidiwa.

Walisema sababu ya kuzuia jeneza lililokuwa limebeba mwili huo ni kwa kuwa wazazi wake walishindwa kumsaidia pale ali[1]pohitaji msaada kiasi cha majirani kuingia jukumu la kumsaidia mahali pa kuishi ingawa bado chakula pia hakuwa anakipata.

“Tulizuia maiti isiingie ndani kwa wazazi wake kwa sababu tu[1]likuwa tunajua maisha anayoishi. Msaada wake mkubwa ulitoka kwa majirani wakati wazazi wake wana uwezo, sasa tukasema kama hawakumsaidia mwanzo wat[1]uachie wenyewe,” alisema mmoja wa majirani zake ambaye haku[1]penda kutaja jina lake.

Jirani mwingine ambaye wa[1]zazi wake walimpa hifadhi kijana huyo alisema Stahimili ambaye alikuwa pia na matatizo ya kiafya, alikuwa na mgogoro na familia yake na alipokuwa akijaribu kutafuta suluhisho hakusikilizwa.

Kwa mujibu wa jirani huyo, kijana alikwenda nyumbani kwao kuomba msamaha ili kuweka mambo sawa ila mambo yalishin[1]dikana.

Alisema alikuwa akifanya kazi viwandani baadaye kazi iliisha kwa sababu ya matatizo yake ya kiafya (kupoteza fahamu mithili ya kifafa), baadaye alikosa fedha za kula na kulipa kodi akaamua kurudi nyumbani kwao kuomba msaada ila alielezwa hana nafasi kwao labda aende kwa baba yake mdogo.

Baada ya vurugu za wananchi wa eneo hilo la Temeke Maganga kuzuia maiti, iliwekwa nje ya jumba moja bovu alikolazimika kuishi, jirani na nyumbani kwao na kuagwa.

Lakini wazee wa busara na viongozi wa dini walituliza hali, kukawa tulivu. Wakati wa kupeleka mwili kwa ajili ya kuupumzisha kwenye nyumba yake ya milele katika Makaburi ya Wailes, Chang’ombe wananchi walizuia pia asibebwe na gari lililokuwa limekodiwa na wao wakaamua kuubeba wenyewe.

Baba wa kijana huyo, Beda Malya alikataa kuzungumzia saka[1]ta hilo huku mama yake mzazi, Segolina Alphonce aliyekuwa akiishi Moshi, Kilimanjaro na ambaye alikuja kwa ajili ya msiba wa mtoto wake akisema mwanaye alikuwa akiishi na baba yake tangu akiwa na umri wa miaka saba na hakujua lolote linaloendelea ila anamwachia Mungu.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Temeke kwa Maganga, Jaffar Shoo alisema sio vizuri kutoa hukumu kwa wazazi wa kijana huyo na kwamba watafanya uchunguzi wa kile kinachoelezwa kama ni kweli ila anachoamini kijana huyo ni mtu mzima na hakuna aliyemlazimisha kujiua isipokuwa siku yake imefika.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Ju[1]manne Muliro alisema atafuatilia sakata hilo kujua kinachoendelea.

 

Habari Zifananazo

Back to top button