Majogoo vs Mashetani kuumana EPL

ENGLAND: LIGI Kuu nchini England (EPL) leo mtoto hatumwi dukani, Majogoo wa Anfield Liverpool watakuwa wageni wa Mashetani Wekundu, Manchester United katika Uwanja wa Old Trafford majira ya Saa 11:30 jioni.

Wakiwa tayari wameshacheza michezo 30, Liverpool wapo nafasi ya pili ya msimamo wa EPL wakiwa na jumla ya alama 70 , ilhali United wapo nafasi ya sita wakiwa na jumla ya alama 48.

United wanaihitaji zaidi mechi hii ili walau kufufua matumaini ya kuingia kwenye nafasi nne za juu.

Mchezo wa mwisho kukutana ni katika michuano ya Kombe la Ligi (FA) mnamo Machi 17 mwaka huu, United wakaibuka na ushindi wa 4-3.

Kuelekea katika mchezo huu, makocha wa timu zote mbili wamezungumza, mwenyji Erik Ten Hag amewaasa mashabiki wa United kuhamasika kushangilia klabu hiyo.

Upande wake, mwalimu wa Liverpool Jurgen Klopp amewataka wachezaji wake kujituma zaidi ili kupanda kileleni mwa EPL, nafasi inayokaliwa na Arsenal wenye alama moja na mchezo mmoja mbele.

Habari Zifananazo

Back to top button