Makalla: Samia ameboresha sekta ya afya Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mapinduzi makubwa kwenye sekta ya afya mkoani Arusha, huku Hospitali ya Wilaya ya Meru Wilayani Arumeru ikipokea shilingi Milioni 900 zilizotolewa kuboresha miundombinu ya huduma za afya hospitalini hapo.
CPA Makalla ameeleza hayo leo Septemba 09, 2025 alipotembelea na kukagua hali ya utoaji na upatikanaji wa huduma kwenye majengo mapya manne ya Hospitali hiyo ikiwemo Jengo la wagonjwa wa nje, Jengo la Maabara, Jengo la Bohari ya dawa, jengo la kuchomea taka pamoja na jengo la wagonjwa wa dharura.
SOMA: Rais Samia amefanya makubwa huduma za afya Meru
Majengo hyao tayari yameanza kutoa huduma kwa wagonjwa, yakitajwa kupunguza muda wa utoaji wa huduma kwa mgonjwa kutoka saa nane hadi mbili.
“Faida za uwekezaji huu mkubwa ni pamoja na kupunguza masaa ya kuwahudumia wagonjwa kutoka saa nane mpaka saa mbili, uwepo wa vipimo 38 ambavyo vimepunguza rufaa za wagonjwa kwenda kwenye hospitali za rufaa kama vile KCMC na Mount Meru.
Haya ni mafanikio makubwa kwa serikali yetu, niwaombe watoa huduma wote kupitia uwekezaji na maboresho haya, vitafsiriwe kwa ninyi kutoa huduma bora kwa wagonjwa, kuanzia mapokezi, lugha nzuri mpaka kwenye huduma za matibabu,” amesema CPA Makalla.
Aidha, CPA Makalla, amesisitiza kuwa, mapinduzi hayo makubwa kwenye sekta ya afya yameambatana na ongezeko kubwa la bajeti kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo pamoja na ukarabati wa jengo la watoto njiti na watoto wachanga wenye kuhitaji uangalizi maalumu.
Awali akisoma taarifa ya Hospitali hiyo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt Elisante Fabian licha ya kumuahidi Mkuu wa Mkoa utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa wa Meru na maeneo ya jirani, ameeleza faida za maboresho hayo kuwa ni pamoja na kuongeza wigo wa utoaji wa huduma na idadi ya wagonjwa na ongezeko la mapato ya Hospitali.
Google pays $300 on a regular basis. My latest salary check was $8600 for working 10 hours a week on the internet. My younger sibling has been averaging $19k for the last few months, and he constantly works approximately 24 hours. I’m not sure how simple it was once I checked it out.
This is my main concern………………. http://Www.Cash43.Com