Makarani waapishwa uchaguzi mkuu

MTWARA: MAKARANI waongozaji wapiga kura zaidi ya 600 wameapishwa katika Jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025

Akifungua zoezi hilo la kiapo kwa makarani hao, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Tandahimba Ramadhani Mmbughu amesema lengo kiapo hicho ni kuwapitisha makarani hao katika majukumu ya ikiwemo utoaji wa huduma mzuri kwa wapiga kura.

Kiapo hicho yamefanyika leo Oktoba 25, 2025 kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mkoani humo, jimbo ambalo lina kata 32 huku vituo vya kupigia kura vikiwa 569.

Pia makarani hao wamekumbushwa suala la utunzaji wa siri, kuzingatia muda wa kuripoti eneo la kituo cha kupigia kura ambao ni saa 1 kamili asubuhi ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima wakati wote wa upigaji kura.

“Lakini pia tunawaasa wananchi wa jimbo hili laTandahimba kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya Oktaba 29 mwaka huu Kwa ajili ya kutimiza takwa lao la katiba kuchagua kiongozi wanaomtaka”amesisitiza

Akitoa mada wakati wa kiapo hicho, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Naputa kwenye Halmashauri hiyo Subiri Mlaponi amesema wajibu na majukumu ya makarani hao ikiwemo kutoa kipaumbele kwa wapiga kura wenye mahitaji maalumu kama vile wazee.

“Makundi mengine yanayotakiwa kupewa kipaumbele ni akina mama wajawazito, walemavu lakini pia kuwapokea wapiga kura nje ya kituo na kuwaekekeza chumba cha kupigia kura”amesema Mlaponi

Baadhi ya washiriki wa kiapo hicho akiwemo Goreth Aloyce kutoka kata ya Tandahimba amesema kupitia kiapo hicho ataenda kutekeleza majukumu hayo kwa kuzingatia sheria.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button