Makinda ataka uhalisia takwimu za kilimo, mifugo

KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Anne Makinda ametoa mwito kwa vijana watakaofanya utafiti wa kilimo na mifugo wakusanye takwimu halisia zitakazosaidia kuleta maendeleo ya kweli kwa Taifa.
Makinda amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya wasimamizi na wadadisi wa utafiti wa kilimo na mifugo kwa mwaka 2024/2025 mjini Morogoro juzi. Amehimiza wananchi wawape ushirikiano vijana hao katika maeneo yao yaliyoteuliwa kwa kutoa taarifa za ukweli kuhusu hali yao ya kilimo na mifugo ili serikali iweze kujipanga ni namna kuimarisha sekta hizo. “Nawaomba wananchi watoe ushirikiano, ni muda mfupi unatumika isipokuwa waseme mambo ya kweli ili yaweza kusaidia kesho yake,” alisema Makinda.
Vijana 250 waliohitimu elimu ya vyuo vikuu wamepatiwa mafunzo ya usimamizi na udadisi wa utafiti wa kukusanya takwimu kwa miezi miwili kuhusu uzalishaji katika kilimo na mifugo. Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Daniel Masolwa amesema takwimu bora ni msingi wa sera bora hivyo wadadisi hao wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, umahiri na weledi.

“Hatutatarajia kuona wanakwenda kukusaya taarifa ambazo hazina ubora unaokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa bali wanatumia mafunzo haya kukusanya taarifa sahihi,” alisema Msolwa. Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Kilimo, Joseph Kiraiya amesema takwimu zitakazopatikana zitaonesha uhalisia wa hali ya sekta ya kilimo kwa maana ya uzalishaji kwa baadhi ya mazao.
Kiraiya amesema takwimu nyingine zinazotumika zinazotokana na sensa ya kilimo zinazofanyika kila baada ya miaka 10 na akabainisha kuwa sensa ya mwisho ya kilimo nchini ilifanyika mwaka 2019/2020 na inatarajiwa kufanywa nyingine 2030. “Wadadisi hawa wanaenda maeneo mbalimbali na wanachagua aina ya mazao ya kilimo na kuona uzalishaji wake, tija yake, upatikanaji wa mbolea, upatikanaji wa fedha ya kilimo,” alisema.
Mtakwimu Mkuu na Mkufunzi ngazi ya Taifa katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Da Silva David Mlau amesema takwimu ni dhana kubwa ambayo inahitaji mtu mwenye ujuzi ili kuzikusanya kwa usahihi na kwa wakati. SOMA: Mbolea ya ruzuku itumike nchi zote EAC kukuza uzalishaji





Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com
Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
.
Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com