Makonda aagiza viwanda kuongeza thamani mazao

ARUMERU, Arusha: MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru kubuni mpango wa kuwezesha ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo ili kuongeza tija kwa wakulima na wafugaji wanaopatikana wilayani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda

RC Makonda ametoa agizo hilo leo wakati alipofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha na kuzungumza na watendaji wa wilaya hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea wilaya zote sita za Mkoa wa Arusha.

SOMA: Makonda aahidi raha wanyonge Arusha

Ameiagiza halmashauri hiyo pia kutafuta mazao ya kimkakati yatakayoitambulisha wilaya hiyo akishauri nguvu kuwekezwa kwenye kilimo cha mazao yanayotumika kwenye kutengeneza marashi kwani tafiti zinaonesha kuwa ardhi ya Wilaya ya Arumeru inafaa kwa kilimo hicho.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Jeremia Kishili, ameagizwa na Mkuu wa mkoa kuundwa kwa mkakati maalum wa kuvutia sekta na watu binafsi kuwekeza kwenye nyumba za kulala wageni na watalii mbalimbali hasa kwa wale wanaotumia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) kuingia nchini Tanzania.

Habari Zifananazo

Back to top button