Makonda aahidi raha wanyonge Arusha

ARUSHA; MKUU wa Mkoa wa Arusha , Paul Makonda ameahidi kujenga heshima yake kwa kurejesha haki kwa wananchi walionyang’anywa na hatakubali kuona vilio vya wananchi wa Arusha waliokata tamaa kutokana na kero zao kutotatuliwa.

Pia amesema wananchi wanaohitaji haki, lakini wamekosa fedha za kuwalipa mawakili, atawaomba wanasheria wa serikali kupitia Chama cha Mawakili nchini (TLS), ili wawasaidie wapate haki zao mahakamani walizodhulumiwa.

Ametoa kauli hiyo leo, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Arusha waliojitokeza kwenye kliniki ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi , tukio lililoshirikisha wanasheria na wadau wa masuala ya ukatili ikiwemo migogoro ya kazi na ajira

Amesema hawezi kukaa kwenye kiti cha ukuu wa mkoa, huku wananchi anaowaongoza wakiteseka na changamoto mbalimbali ambazo zipo ndani ya mamlaka yake ya kiuongozi.

“Nimeita kliniki hii kwa ajili ya kusaidia wananchi wenye changamoto zao na nyie mnaohudumia wananchi ambao ni watumishi wa umma toeni huduma kwa wananchi kwa kutoangalia waliovaa vizuri, vimemo au kujuana, kila mwenye shida atatuliwe msiwabague,” amesema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button