Makonda amsifu Dk Samia utunzaji amani

Na Rehema Lugono,Arusha

MGOMBEA wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Paul Makonda amesema mgombea wa urais kupitia chama hicho, Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha uongozi wake ameonyesha kwa vitendo uwezo wake wa kulifanya taifa kubaki salama kwa kukabiliana na changamoto zinazoweza kuligawa taifa.

Makonda alisema hayo mtaa wa Majengo ya Juu, Arusha wakati alipokuwa akifanya ziara ya mtaa kwa mtaa kumuombea kura Samia,wagombea udiwani na ubunge wa chama hicho.

“Samia ameonyesha kwa vitendo anavyoweza kukabiliana na changamoto zinazoweza kulipasua taifa na kuligawa lakini katuonyesha uwezo wake wa kukisimamia taifa kubaki imara kwa kiwango cha kwamba Tanzania bado ni ile ile aliyoiacha Hayati Julius Nyerere ya watu wanaoishi bila kuulizana kabila wala dini,”alisema Makonda.

Alitoa wito kwa Watanzania kujiuliza ni mataifa mangapi yaliyoweza kustahimili kuwa na amani mara baada ya kiongozi wao kufariki akiwa madarakani,Samia ameweza kulibeba taifa likabaki kuwa na umoja hata kwenye majanga makubwa ikiwemo kipindi cha UVIKO 19 wakati biashara zzilyumba na uchumi wa taifa ulishuka.

“Lazima tunapoenda kupiga kura tukamchague kiongozi ambaye tunajua yapo mambo ambayo tunajua kiongozi huyu jambo hili anauwezo nalo,moja ya jambo muhimu la kumpima kiongozi tunayeenda kumchagua kwamba uwezo wake upoje wakati nchi inavyopitia changamoto,”alisema.

Makonda alisema lazima wajiulize je kiongozi wanayemtaka ikitokea siku Tanzania haina mazungumzo mazuri na nchi majirani ana uwezo wa kulilinda taifa na kusuluhisha mgogoro huo kwa njia ya amani.

“Niwathibitishie kuwa Samia ana sifa hizo zote na ana uwezo mkubwa wa kuongoza nchi kwa demokrasia huru.Amani ni muhimu ikashatoeka hakutakuwa na amani ya mbadala tusimamie na tulinde amani yetu kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita inavyohakikisha nchi inasalia kuwa na amani, tangu uhuru hatujawahi kusikia Tanzania imetofautia na nchi nyingine,”alisema.

Aliwaomba wananchi kumchagua Samia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu ya utu,utulivu,msikivu na mstahimilivu nyakati zote.

Alimsifu Samia kwa utekelezaji wa mradi wa Reli ya Kisasa ya (SGR), akisema uwekezaji huo umeonyesha kwa vitendo ubora na umakini wa Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha wananchi wanasafiri kwa usalama na uhakika.

Alifafanua kuwa hivi karibuni SGR iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma ilipata hitilafu na baadhi ya watu kutangaza kwenye mitandao ya kijamii kwamba treni hiyo imepata ajali.

Alisema hata hivyo kutokana na ubunifu na teknolojia ya kisasa iliyowekezwa na serikali, ndani ya masaa mawili na nusu tu treni nyingine ya mchongoko ililetwa na kuendelea na safari, na hakuna abiria hata mmoja aliyeshindwa kufika Dodoma au Dar es Salaam kwa njia ya SGR.

“Huu ndio ushahidi wa uongozi makini wa Samia Suluhu Hassan.Kipindi cha nyuma behewa moja likidondoka, treni ilikuwa inasimama siku kadhaa; mvua ikinyesha kidogo reli inateleza na abiria wanakwama porini lakini leo hii, ndani ya muda mfupi tu, tatizo linatatuliwa na safari zinaendelea kama kawaida,” alisema.

Makonda alisisitiza kuwa mafanikio hayo ni kielelezo cha Tanzania mpya yenye mifumo imara ya usafiri, inayotokana na maono ya Samia katika kuboresha miundombinu na huduma kwa wananchi.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

    1. I­ g­­­­­e­t­­­­ p­a­i­­­d­­­­­­­ o­­­­­v­e­r­ 2­­­2­­­0­­­ D­­­o­­­­­­lla­­­r­­­­­s p­­­­­e­­­­­r­ ­­­h­o­­­­­u­r­­­ ­­­­w­­­­o­r­k­­i­­­­n­g­ f­r­o­­m­ h­o­m­e­ ­w­i­t­h­­ 2 k­i­d­­s­ a­t­ h­o­­m­e­. i­ n­e­v­e­r­ t­h­o­u­g­h­t­ i­’d­ b­e­ a­b­l­e­ t­o­ d­o­ i­t­ b­u­t­ m­y­ b­e­s­t­ f­r­i­e­­n­d­ e­a­r­­n­s­ o­v­­e­r­ 1­5k­ a­ m­­o­n­t­h­ d­­o­i­n­g­ t­h­­i­s­ a­n­d­ s­­h­e­ c­o­n­v­i­n­c­­e­d­ m­e­ t­o­ t­r­­y­. it was all true and has totally ch­a­n­g­e­d­ ­m­y­ l­i­f­e­. T­h­i­s­­ ­i­s­ ­w­h­a­t­­ ­I­ ­d­­o­­­­­­­,­­­­­­­ ­c­h­­­­­e­­­­c­­­­k­ ­­­­i­­­­t­ ­o­­­­­u­t­ ­­­­b­y­ ­­­­V­i­s­­­­­i­t­i­n­­­­g ­F­o­­­­l­l­o­w­i­­n­­­­­g ­W­e­b­s­­­­­i­t­e

      ­
      Open This….  http://Www.Work99.Site

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  3. I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
    Try it, you won’t regret it!….. https://www.Homeprofit1.site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button