Makonda ataka uhamasishaji upandaji miti

ARUSHA: MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameagiza mamlaka zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi ikiwemo watu wa mazingira kuhakikisha wanakagua wananchi na wawekezaji wanaoomba vibali kwa ajili ya ujenzi wa makazi na maeneo mengine kupanda miti ili kulinda mazingira.

Aidha amesema wenyeviti bora wa serikali za mitaa au vijiji kutoka halmashauri tatu wanaohamasisha wananchi kupanda miti na usafi wa mazingira watapewa zawadi ambapo mshindi wa kwanza atapata kiasi cha Sh milioni 5 mshindi wa kwanza mshindi wa pili Sh milioni 3 na wa tatu Sh milioni 2 kama motisha kutoka Benki ya CRDB kila mwezi.

Advertisement

Rc Makonda ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti eneo la Shangarai wilayani Arumeru Mkoani Arusha katika barabara kuu ya Moshi-Arusha huku wananachi , viongozi na wadau mbalimbali wakipanda miti zaidi ya 1200 katika eneo hilo la barabara.

Halmashauri hizo ambazo zitashiriki shindano hilo kuanzia Machi 15 mwaka huu ni Jiji la Arusha, Halmashauri ya Arusha na Halmashauri ya Meru.

Amesema mamlaka husika zinazotoa vibali vya ujenzi kwenda kuhakiki maeneo ya upandaji miti ilu kufanya eneo husika kuwa la kijani ikiwemo kutunza mazingira.

Pia ameshauri Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura )na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) kuhakikisha wanapojenga barabara katika maeneo yote wapande miti ili kulinda mazingira huku akiwasihi wenyeviti wa serikali za mitaa katika ofisi zao pamoja na mabalozi wa mitaa mbalimbali kuhakikisha wanafanya usafi na kutunza mazingira

“Mabalozi nanyi mnafungu lenu katika kuhakikisha mnafanya usafi na kupanda miti na kila balozi atapata motisha yake sasa ataamua kula na kunywa na wananchi wake ambao wameongoza katika suala zima la usafi kwani Machi 15,mwaka huu fedha hizo zitatolewa kwa wale wanaoongoza kwa kufanya usafi vizuri”

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *