Makonda atimiza ahadi yake kwa Prof. Jay
DAR ES SALAAM: Katibu wa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda ametimiza ahadi yake ya kumchangia Sh milioni 10 aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi na Mwanamuziki wa (HipHop), Joseph Haule Maarufu Professor Jay.
Makonda ametimiza ahadi hiyo alipofika nyumbani kwa, Professor Jay Mbezi Jijini Dar es salaam.
Pia, Mwenezi Makonda amemkabidihi Professor Jay kiasi kingine cha fedha Sh milioni 10 ikiwa ni mchango kutoka kwa ndugu wa zake na kupelekea kuwa amekabidhi jumla ya Sh milioni 20.
Akizunguma na Makonda, Professor Jay amebainisha changamoto ya umbali anayoipata kutoka Mbezi hadi kufika Hospitali ya Muhimbili ambapo Makonda amemuahidi kumtafutia nyumba na kumlipia eneo la Upanga ili kusudi kuepukana na changamoto hiyo anayoipitia.