Mama Dangote wa Same adakwa kilimo cha mirungi

KILIMANJARO: MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, imefanya operesheni maalum wilayani Same, mkoani Kilimanjaro kuanzia Machi 19 hadi 25, 2025.

Katika operesheni hiyo, ekari 285.5 za mashamba ya mirungi zimeteketezwa na watuhumiwa saba wamekamatwa, akiwemo anayedaiwa kuwa kinara wa biashara haramu ya mirungi nchini aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu, Interindwa Zinywangwa Kirumbi, maarufu kwa jina la mama Dangote.

Akizungumza baada ya operesheni hiyo, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amedai kuwa, mama Dangote ni mzalishaji na msambazaji mkubwa wa dawa za kulevya aina ya mirungi nchini.

Amedai kwa zaidi ya miaka 30, amekuwa akiendesha mitandao ya biashara haramu ya mirungi na kusimamia masoko ya dawa hizo za kulevya katika maeneo mbalimbali nchini, licha ya kujua kuwa ni kinyume cha sheria.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button