Man Fongo kutetea haki za wanawake watoto

MSANII wa singeli Man Fongo ameweka wazi kuwa anaandaa nyimbo zenye ujumbe maalum wa kutetea haki za Wanawake na Watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Man Fongo amesema hayo katika mjadala ulioandaliwa na UNICEF kwa kushirikiana na Sauti za Busara, uliojikita katika namna wasanii wanavyoweza kutumia sauti na ushawishi wao kukemea ukatili na kutetea haki za wanawake na watoto.

Mjadala huo uliwakutanisha wasanii, wadau wa sanaa na wataalamu wa ulinzi wa watoto kutoka UNICEF, kwa lengo la kuhimiza utengenezaji wa kazi zitakazoishi vizazi na vizazi. SOMA: Dulla Makabila aweka rekodi mpya

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button