Man Water: Mpango wa kumrudisha 20% upo pale pale

MTAYARISHAJI wa muziki kutoka studio ya Combination Sound, John Shariza maarufu Man Water amesema mpango wake wa kumrudisha msanii, Abbas Kunzasa maarufu 20 Percent bado upo pale pale.

Man Water na 20 Percent waliwahi kufanyakazi pamoja na nyimbo walizofanya pamoja zikashinda tuzo tano za muziki Tanzania lakini baada ya hapo wakatofautiana na baadae wakatangaza kufanyakazi tena pamoja.

“Lengo la kumrudisha 20 Pencent bado lipo, kwa sasa linasubiri muda tu ili watu waone kwa vitendo maana maneno hayatakiwi kuwa mengi bali vitendo,” ameeleza Man Water.

Ujio mpya wa Man Water na 20 Percent aliyewahi kuwika na nyimbo mbalimbali ukiwemo ‘Mama Neema’, ‘Money Money’, ‘Mali za Urithi’, ‘Subira’ na ‘Inachoma’ unasubiriwa mno na mashabiki wao kutokana na mashabiki hao kutamani kusikia ujumbe aliokuwa akiuandika 20 percent katika nyimbo zake.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button