Mapitio kada ya afya kukamilika Mei

NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema, wizara hiyo inakamilisha mapitio ya miundo ya kada za afya ambayo yanatarajiwa kukamilika mwezi Mei mwaka huu.

Amesema baada ya kazi hiyo kukamilika, yatawasilishwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala na Bora kwa ajili ya kupata idhini ili watumishi wa afya waanze kunufaika kutokana na maboresho hayo.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Aprili 28, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Dkt. Alice Kaijage katika mkutano wa kumi na moja kikao cha 15 Bungeni jijini Dodoma.

“Wizara inakamilisha Mapitio ya Miundo ya kada za afya, kazi ambayo inatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2023 na kuwasilishwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala na Bora kwa ajili ya kupata idhini.” Amesema Dkt. Mollel

Amesema,  kukamilika kwa maboresho ya miundo hiyo kutasaidia kukidhi mahitaji ya kiutumishi kwa wataalamu mbalimbali wa afya wakiwemo Madaktari Bingwa na Wataalamu wengine waliopata fursa ya kujiendeleza katika kada zao.

Habari Zifananazo

Back to top button