Marco wa Zabron Singers afariki dunia

DAR ES SALAAM: MWIMBAJI wa kundi la Zabron Singers maarufu Marco, Joseph amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Agosti 22 katika Taasisi ya Moyo wa Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na Daily News Digital mwenzake Japhet Zabron amethibitisha kutokea kwa kifo cha msanii huyo.

“Ni kweli Marco Japhet amefariki ghafla tu mshtuko wa moyo alianza Jumapili iliyopita ukiachana na Jumapili hii na alikuwa hasumbuliwi chochote kipindi cha nyuma imekuaa gafla,”

Nyimbo za dini alizowahi kutoa kipindi cha uhai wake ni Upo Single, Fundi, Tofauti na Daktari.

Habari Zifananazo

Back to top button