Mashabiki wa soka kushindania dau nono

ILI kuhamasisha Watanzania wengi kuendelea kufuatilia michuano ya Kombe la Dunia, Betway Tanzania imeungana na Airtel Tanzania kutambulisha shindano la ubashiri ambazo zitawawezesha wapenzi wa soka wanaofuatilia Kombe la Dunia kujishindia zawadi mbalimbali.

Akizungumza Dar es Salaam leo Novemba 29, 2022 , Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe amesema shindano hilo limepangwa kufanyika kwa kipindi chote cha michuano hiyo ambayo imeingia robo fainali na itawanufaisha washiriki kwa kutoa zawadi ya kila siku ya fedha taslimu Sh 10,000 kwa washindi 50, watu 50 watakuwa na nafasi ya kushinda Sh 10,000 kila siku.

“Zawadi ya kila wiki ya fedha taslimu Sh 1,000,000 kila wiki mtu mmoja atakuwa na nafasi ya kuibuka na kitita cha Sh 1,000,000. Hii ina maana kwa kipindi kilichosalia cha mashindano angalau watu wanne wana nafasi ya kushinda zawadi ya pesa taslimu ya Sh 1,000,000,” alisema Masaoe.

Amesema pia kuna zawadi kubwa ya Sh 5,000,000, mshindi wa jumla anatarajiwa kukusanya jumla ya Sh 5,000,000 zitakazotolewa baada ya fainali ya Kombe la Dunia.

Aliongeza kuwa mbali na zawadi za pesa taslimu, mashabiki wa michezo pia wana nafasi ya kupata dau la bure la kuwasaidia kubashiri bila malipo na itaongeza nafasi za mashabiki wengi zaidi kushiriki katika shindano na kuibuka mshindi wa kila siku, mshindi wa wiki au mshindi wa jumla.

“Kwa wateja wetu wapendwa wa Betway, hii ni nyongeza. Ni faida ya ziada kwa wateja wanaotumia Airtel Money kwa sababu wanaweza kujishindia zawadi kadha wa kadha kadiri wanavyobashiri nasi kupitia Airtel Money,” amesema Masaoe.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Airtel Mone, Isack Nchunda amesema watumiaji wa huduma za Airtel Money wanaweza kupata kilicho bora zaidi katika Kombe la Dunia kwa kutabiri matokeo katika hatua zote za mashindano hayo.

“Tumefurahi sana kushirikiana na Betway Tanzania kwa sababu tunajua kupitia ushirikiano huu watumiaji wetu wa huduma ya Airtel Money wanaopenda michezo watanufaika moja kwa moja na Kombe la Dunia.

”Lengo letu ni kuhakikisha wateja wetu wanapata kilicho bora zaidi kutoka kwenye huduma zetu katika kipindi hiki muhimu ambacho macho ya ulimwengu mzima yako kwenye michuano hiyo, tunatamani kuona wateja wetu wakinufaika na Kombe la Dunia na tunaamini hii ni njia mojawapo ya kuwasaidia,” amesema Nchunda.

Aliongeza kuwa shindano hilo pia ni sehemu ya ofa za msimu wa sikukuu kutoka kwa kampuni hiyo ya mawasiliano ya simu kwani Airtel imedhamiria kusherehekea msimu wa sikukuu na wateja wake wapendwa.

Huku timu tatu pekee zikiwa zimefuzu kwa hatua ya 16 bora hadi jana, mashabiki wa michezo bado wanaweza kufanya ubashiri wao katika michezo inayoendelea ya hatua ya makundi ili kujiwekea nafasi ya kushinda zawadi. Zawadi kuu ya Sh 5,000,000 itatolewa kwa mshindi Desemba 31 baada ya mchezo wa fainali utakaochezwa Desemba 18, 2022.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x