Mashamba ya kahawa Kagera kupimwa kidigitali

KAGERA: Kampuni ya Bizy Tech kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) imeanza utekelezaji wa mpango wa utambuzi wa kusajili mashamba ya wakulima wa kahawa pamoja na wakulima kidigitali mkoani Kagera.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Utunzaji wa Mazingira ya Jumuiya ya Ulaya.

Ofisa Mkuu wa Kampuni hiyo, Rahim Shoo akitoa mafunzo kwa wasajili wa zoezi hilo maofisa kilimo ,wadau wa kahawa halmashauri za Mkoa wa Kagera amesema usajili wa mashamba kidgatali unalenga kuhimiza utunzaji wa mazingira ya asili na kulinda uoto wa asili kama yalivyokuwa makubaliano na Jumuiya za ulaya.

Amesema kuwa zoezi litaanganzia mashamba yote ya wakulima huku likienda sambamba na swala la utunzaji wa uoto wa wasili na kulinda mazingira hasa kwa wanaoharibu mazingira wanapotaka kuanzisha mashamba mapya huku akidai kuwa hii ni fursa muhimu kwa wanaotaka kuuza kahawa yao Ulaya.

“Kumekuwa na vikwazo vingi pale tunapotaka kupeleka kahawa yetu katika soko la Ulaya ,kule ndiko Kuna pesa moja ya changamoto ni swala la ulinzi wa mazingira serikali yetu imeamua sasa kutumiza matakwa ya masoko ya kidunia Kwa kufanya usajili wa kidgtali ambao unabaini uharibufu wa mazingira hasa kwa mashamba ambayo yameanzia mwaka 2021 mpaka sasa,” amesema Shoo.

Amesema zoezi hilo litafanyika katika Halmashauri zote za Mkoa wa Kagera ndani ya miezi mitatu ambapo Wataalamu wa kilimo watahusika moja kwa moja kufanya zoezi hilo na vijana ambao wameteuliwa na serikali wanaojuna kutumia vifaa vya kidigitali wamepata fursa hiyo ya ajira kwa miezi mitatu mfululizo

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa amepongeza mpango huo na kudai kuwa serikali imeupokea kwa mikono miwili na Kutaka watakaoshiriki zoezi Hilo kufanya kazi kwa weledi na kukamilisha zoezi Hilo kwa wakati huku akidai kuwa zoezi la Kuanzisha mashamba mapya ya Kahawa halitaathiri mazingira Na uoto wa asili

Amesema Kahawa ambayo inalimwa kwa uharibifu wa mazingira haiuziki Dunia huku akipiga marufuku watu wenye Nia ovu ambao watakuja kupotosha zoezi Hilo lenye Nia njema.

“Najua Kuna watu wanapita wanawaambia mashamba yenu yatachukuliwa ,mashamba yenu yatauzwa tuwapinge hawa watu ,kwanza zoezi hilo litatusaidia kujua aina ya wakulima tulio nao na mahitaji yao halisi , uwezo wa mashamba yetu na aina ya miche inayopaswa kuzalisha na sisi kama serikali tunapoenda Kuanzisha mashamba mapya tayari tutayaanzisha bila kuathiri mazingira”alisema Mwassa

Meneja wa Bodi ya kahawa kanda ya Kagera Edmond Zani alisema kuwa zoezi Hilo litakapokamilika litakuwa limechangia upatikanaji wa data kamili na Kubaini nani amiliki shamba kwa kiasi Gani ambapo serikali itapata mwanga mzuri wa kuhudumia wakulima wake pamoja na Kubaini huduma zinazohitajika

Amesema kwa data zisizo rasmi sasa Mkoa wa Kagera unakadiliwa kuwa na wakulima wa zao la kahawa wapatao 250,000 huku hekari za kulima kahawa zikikadiliwa kuwa ni 176,000 ambapo zoezi Hilo litatoa sura halisi na takwimu sahihi zinazohusu maswala ya kilimo cha kahawa zilizopo kwa sasa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button