Mashambulizi Gaza yatikisa huduma za afya

GENEVA : MKURUGENZI  Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameonya kuwa mashambulizi ya ardhini yanayoendelea kufanywa na Israel katika eneo la kaskazini mwa Ukanda wa Gaza yamesababisha hospitali zilizokuwa tayari zimeelemewa kufikia ukingo wa kuporomoka.

Kupitia taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa kijamii wa X, Ghebreyesus alieleza kuwa mashambulizi hayo aliyoyaita ya  kinyama pamoja na  amri ya kuwahamasisha watu kaskazini mwa Gaza yameendelea kuongeza madhara makubwa kwa wakimbizi wa ndani.

Amesema familia nyingi zimejikuta zikiishi katika maeneo  madogo yasiyo na heshima kwa utu wa binadamu huku zikikabiliwa na msongo wa kisaikolojia. SOMA: WHO : Tutaendelea kubaki Gaza

Wakati huo huo, Mwanasheria Mkuu wa Uhispania ametangaza kuwa nchi yake inaanza uchunguzi kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea Gaza, ili kuisaidia Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Taarifa rasmi ya ofisi hiyo imesema kikosi maalum kimeundwa kwa ajili ya kukusanya na kuwasilisha ushahidi utakaosaidia mchakato huo, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza wajibu wa Uhispania katika kushirikiana kimataifa na kulinda haki za binadamu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button