Mashauri 326 ya mirathi yakamilika Morogoro

MOROGORO: MAHAKAMA Kuu Kanda ya Morogoro imeweka kupaumbele katika usikilizaji wa mashauri ya mirathi kwa kuunda kamati ya ufuatiliaji wa kufunga mashauri hayo na kuwezesha kumaliza mashauri 326 kati ya mashauri  567 yaliyofuguliwa nkwenye mahakama mbalimbali za mkoa huo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda hiyo, Rose Ebrahim amesema hayo katika hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini.

Maadhimisho hayo yalifanyika katika Kituo Jumushi cha Utoaji Haki cha Mahakama Kuu Kanda hiyo yakiwa yamebeba kauli mbiu: ‘Mchango wa mahakama katika ustawi na maendeleo ya taifa’.

Jaji Mfawidhi amesema kamati hiyo ilianza kazi Machi 2025 na kufanya jukumu hilo kwa mwaka mmoja hadi Desemba mwaka jana.

Kamati ya ufuatiliaji wa kufunga mashauri hayo ilikuwa chini ya mwenyekiti wake Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Gairo , Irene Lyatuu na mratibu wa kamati hyo ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Morogoro, Janeth Kinyage.

Jaji Mfawidhi amesema wakati kazi hiyo inaanza kulikuwepo na mashauri ya mirathi 567 yalifunguliwa na watu , ambapo kamati hiyo ili maliza mashauri 326 hadi kufikia Desemba 2025 na kubakiwa na mashauri 241 yaliyovuka mwaka 2026.

Amesema utaratibu wa sasa msimamizi wa mirathi anahitaji kufungua akaunti maalumu ambayo itahifadhi fedha zote za marehemu ambapo mgawayo utafanyika chini ya usimamizi wa Mahakama na hiyo itaondoa mlolongo na ucheleweshaji wa malipo katika kesi za mirathi.

“Na katika kuweka utaratibu unaofanana na usikilizaji wa mashauri ya mirathi kwenye Mahakama za Mwanzo kanuni zinamtaka msimamizi wa mirathi kuanzia sasa kufungua account maalumu ya mirathi (special account) katika Benki yoyoyote ya biashara,” amesema Jaji Mfawidhi Rose .

“Akaunti hiyo ni kwa ajili ya kukusanya na kugawa fedha za marehemu chini ya uangalizi wa mahakama hakuna tena pesa hizi kuzileta mahakamani,”alisisitiza Jaji Mfawidhi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda hiyo pia aliwaomba wadau wa mahakama wakiwemo viongozi kutao elimu kwa wanachi kuhusu upatikanaji wa huduma za kimahakama kwa njia ya tehama ili elimu hiyo iweze kuenea na kutumika kwa wananchi wa kawaida.

Mkuu wa mkoa wa Morogro, Adam Malima ambaye alikuwa mgeni maalumu ameiombaMahakama Kuu Kanda hiyo kufirikia upya kurudisha wiki ya sheria kama ilivyokuwa awali hususani ndani ya mkoa huo.

Malima amesema wiki hiyo ilikuwa ina manufaa makubwa kwa wanachini wenye uhitaji wa msaada wa kisheria tofauti na ilivyo sasa.

“Ni hivyo vyema Kituo jumuishi cha kutoa haki cha Kanda ya Morogoro kiangalie uwezekano wa kurudisha wiki hiyo ili kuendelea kutoa msaada kwa wanachi weye uhitaji kwa kushirikiana na taasisi nyingine za utoaji wa haki,” amesema Malima.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..  www.join.work27.com

  2. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do……………………………………………………………………………………………………………………….  www.join.work27.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button