Mashindano ya magari Afrika kufanyika Iringa

MZUNGUKO wa saba wa mwisho wa mashindano ya magari ya Afrika unaofahamika kama ‘Africa Rally Champion Ship’ Mwaka 2023 yataanza kutimua vumbi kwa siku mbili katika shamba la Asas Matembo, Iringa Vijijini na Shamba la Miti la Saohill, wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Mashindano hayo yanayodhaminiwa kwa mara ya kwanza na makampuni ya Asas yatafanyika kwa pamoja na mashindano ya magari ya Taifa (National Rally Championship) kesho na keshokutwa (Novemba 11-12, 2023) huku uzinduzi wake ukitarajiwa kufanyika leo katika uwanja wa Samora, mjini Iringa.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa magari yatakayoshiriki mashindano hayo mapema leo, Rais wa Chama cha Mbio za Magari Tanzani (AAT), Nizar Vijan alisema jumla madereva 17 wamejitokeza kushiriki mbio hizo.

Vijan amesema kati ya madereva hao, saba wanashiriki mbio za Afrika na 10 mbio za Taifa.

“Na kati ya madereva hao, watano wanatoka Kenya, Uganda na Ufaransa huku wengine wote waliobaki ni madereva wa Tanzania,” alisema.

Amesema kati ya madereva saba wanaoshirki mbio za Afrika, ni wawili tu ndio wanaotokea Tanzania ambao ni pamoja na Gurpal Sandhu na Prince Nyerere ambaye ni mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere.
Wengine kutoka nje ni pamoja na Karan Patel, Jas Mangat, Yasin Nasser, Innocent Bwamiki na Hamza Anwar.

Aliwataja wanaoshiriki mashindano ya Taifa kuwa ni Ahamed Huwel, Manveer Birdi, Randeep Singh, Charles Bicco, Kelvin Taylor, Vishal Patel, Bob Taylor, Hamid Mbata, Sultan Chang’a na Issack Taylor.

Aliyataja magari yatakayotumiwa na madereva hao kuwa ni pamoja na Ford Fiesta, Yundai, Mitsubishi Lancer, Subaru Impreza na Toyota Celica.

Katika kumpa moyo mwanaye na kuyapigia debe mashindano hayo Makongoro Nyerere aliyekuwepo wakati wa ukaguzi wa magari yanayoshiriki mashindano hayo alitoa rai kwa serikali kuangalia uwezekano wa kutenga bajeti kwa ajili ya mashindano ya magari kama inavyofanya katika mashindano mengine.

Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoinua michezo nchini hususani mpira wa miguu akisema wakati umefika kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa pia na bajeti kwa ajili ya mashindano ya magari.

Amesema mchezo wa magari ni moja ya michezo inayofuatiliwa sana duniani na kama uwekezaji wake nchini ukiwa mkubwa unaweza kuleta watalii na wawekezaji wengi hasa kwa kuzingatia kwamba unashirikisha idadi kubwa ya watu wenye vipato vikubwa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
AlmaRankin
AlmaRankin
24 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website________ http://Www.Careers12.com

Last edited 24 days ago by AlmaRankin
Angila
Angila
24 days ago

I get paid over $87 per hour working from home with (Qm)2 kids at home. I never thought I’d be able to do it but my best friend earns over 10k a month doing this and she convinced me to try. The potential with this is endless. 
.
.
.
.
Here’s what I’ve been doing…> > > http://remarkableincome09.blogspot.com

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x